Open top menu
Jumamosi, 31 Agosti 2013
Guardiola ambwaga Mourinho UEFA Super Cup


Kocha wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola ameendeleza ubabe wake kwa Jose Mourinho anayeinoa Chelsea baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup leo.

Guardiola ambaye alikuwa hasimu wa Mourinho alipokuwa anaifundisha Barcelona huku Mreno huyo alipokuwa anaiongoza Real Madrid, liibuka kidedea aliposhinda kwa mikwajua ya penalti 5-4.
Kiungo wa Bayern, Mario Goetze (kulia) akipambana na Frank Lampard
 
Mchezo huo ambao ulikwenda kwa dakika 120 baada ya 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1 na zilizpoongezwa dakika za nyongeza pia miamba hiyo ilipata bao moja kila mmoja na kufanya mchezo huo umalize dakika 120 kwa sare ya mabao 2-2.
 Mario Goetze (kushoto) akimiliki mpira mbele ya Frank Lampard

Mabao ya Bayern yamefungwa na Franck Ribéry dakika ya 47 na  Javi Martínez dakika ya 120+1 wakati yale ya Chelsea yalifungwa na  Fernando Torres dakika ya 8′ na Eden Hazard dakika ya 93.
 Manuel Neuer akishangilia ushindi sambamba na mchezaji mwenzake, Frank Ribery

Waliofunga penalti kwa upande wa Bayern ni David Alaba, Toni Kroos, Philipp Lahm, Franck Ribéry na Xherdan Shaqiri na mikwaju ya Chelsea ilikwamishwa na David Luiz, Oscar, Frank Lampard na Ashley Cole, aliyekosa ni Romeo Lukaku.


Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akifuatilia mchezo huo kwa staili ya kipekee.
Javi Martinez (kulia) akiifungia timu yake bao la pili huku kipa wa Chelsea Petr Cech asijue la kufanya
Chini ya Ulinzi: Franck Ribery (katikati) akiwa na mpira huku akizongwa na wachezaji wa Chelsea
 


Read more