Open top menu
Alhamisi, 31 Oktoba 2013
 SIMBA YABANWA NA KAGERA, WANG’OA VITI, MABOMU YARINDIMA TAIFA

Polisi wakiwafuata mashabiki wa Simba ambao walikuwa wanang'oa viti



 


BAO la beki wa kulia wa Kagera Sugar, Salum Kanoni lilipoteza amani ndani ya Uwanja wa Taifa baada ya mashabiki wa Simba kuanza kung’oa viti hali iliyosababiosha Polisi walipue mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo.

Kagera ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Asimi Tambwe katika kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa njia ya panalti baada ya Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika eneo la hatari.

Kwa sare hiyo hali ya Simba imeendelea kuwa tyete kwani bado wamebaki katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 21 nyuma ya Yanga yenye pointi 22 huku Azam na Mbeya City wakiwa juu kwa pointi 23 kila moja wakitofautiana mabao ya kufunga.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa katika dakika zote kwani timu hizo zilikuwa zikihitaji pointi tatu ili wajiweke sehemu nzuri kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Simba itamalizia mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Ashanti United mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi ya Novemba 2.




Read more
SEPP BLATTER AMPONGEZA JAMAL MALINZI

RAIS mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi ameendelea kupokea salamu za pongezi baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Salamu nyingine za zimetoka kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter ambapo amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo nchini.

Blatter amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini, na kuongeza kuwa milango ya FIFA iko wazi wakati wowote anapotaka kujadili masuala yanayohusu mchezo huo.

“Nakutakia wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu,” amesema Rais Blatter katika salamu zake.


Wengine waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.
Read more
YANGA KUENDELEZA KIPIGO KWA WANAJESHI KESHO?

RAUNDI ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Novemba 1 mwaka huu) kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Tiketi zitauzwa siku ya mechi uwanjani katika magari maalumu kuanzia saa 4 asubuhi.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.


Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Read more
BALE, RONALDO, BENZEMA WAITEKETEZA SEVILLA, WAIPIGA SABA

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Gareth Bale baada ya kuchemsha katika mchezoi dhidi ya FC Barcelona jana alirudi katika kiwango cha hali ya juu na kuisaidia timu yake kuiangamiza Sevilla mabao 7-3 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

Katika mchezo huo Bale aliifungua Madrid mabao mawili huku akitoa pasi za mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa mwiba wa Sevilla katika mchezo huo.

Mabao mengine mawili ya Madrid yalikwamishwa wavuni na Karim Benzema na kuhitimisha ushindi wa mabao hayo saba na kufanikiwa kujiliwaza na kipigo cha Barca.


Mabao ya kufutia machozi ya Sevilla yalifungwa na Ivan Rakitic aliyetupia mabao mawili na bao moja lilifungwa na Carlos Bacca wakati mchezaji wao, Mcameroon Stephane Mbia alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Read more
Jumatano, 30 Oktoba 2013
 SIMBA, KAGERA HAPATOSHI KESHO TAIFA, YANGA NA JKT KESHOKUTWA

LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Read more
YANGA, MGAMBO SHOOTING WAINGIZA MIL 37/-

PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.


Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.
Read more
 HAYATOU AMPONGEZA JAMAL MALINZI

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.


Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.
Read more
UNAWAJUA WANASOKA WANAOWANIA TUZO MWANASOKA BORA WA DUNIA 2013, HAWA HAPA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) limetoa majina ya wachezaji 23 watakaowania tuzo za mwanasoka Bora wa Dunia kwa mwaka 2013 ‘FIFA Ballon d’Or’.

Wachezaji hao 23 waliotangazwa watachujwa mwezi Desemba mwaka huu na kubaki wachezaji watatu ambao wataingia kwenye hatua ya mwisho ya fainali itakayofanyika Januari 13, 2014 jijini Zurich, Uswisi.

Hicho cha kutoa tuzo hiyo pia kutachaguliwa kikosi bora cha mwaka, kocha bora, mchezaji bora wa kike, beki bora, golikipa bora, kiungo na mshambuliaji bora wa dunia.

Majina ya wachezaji hao na nchi zao kwenye mabano ni Gareth Bale (Wales), Edinson Cavani (Uruguay), Radamel Falcao (Colombia), Eden Hazard (Ubelgiji), Zlatan Ibrahimović (Sweden), Andres Iniesta (Hispania), Philipp Lahm (Ujerumani), Robert Lewandowski (Poland), Lionel Messi (Argentina), Thomas Muller (Ujerumani), Manuel Neuer (Ujrumani), Neymar (Brazil) na Mesut Ozil (Ujerumani).

Wengine ni Andrea Pirlo (Italia), Franck Ribéry (Ufaransa), Arjen Robben (Uholanzi), Cristiano Ronaldo (Ureno), Bastian Schweinsteiger (Ujerumani), Luis Suarez (Uruguay), Thiago Silva (Brazil), Yaya Toure (Ivory Coast), Robin Van Persie (Netherlands) na Xavi (Hispania).

Kwa upande makocha waliotajwa katika orodha ya kuwania tuzo ya kocha bora wa dunia nchi zao na timu wanazofundisha kwenye mabano ni Carlo Ancelotti (Italia/Paris Saint-Germain FC/Real Madrid CF), Rafael Benítez (Hispania/Chelsea FC/SSC Napoli), Antonio Conte (Italia/Juventus) na Vicente Del Bosque (Hispania/Timu ya Taifa ya Hispania).


Wengine ni Sir Alex Ferguson (Scotland/Kocha wa zamani wa Manchester United), Jupp Heynckes (Germany/Kocha wa zamani wa FC Bayern München), Jurgen Klopp (Germany/Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Ureno/Real Madrid CF/Chelsea FC), Luiz Felipe Scolari (Brazil/Timu ya Taifa ya Brazil), Arsene Wenger (Ufaransa/Arsenal FC).
Read more
CHELSEA YAIONDOA ARSENAL CAPITAL ONE, MAN UTD YAUA

TIMU ya Arsenal jana imeyaaga mashindano ya Capital One baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa hatua ya mtoano ya michuano hiyo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa vijana wa Jose Mourihno walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa beki wake wa kulia, Mhispania Cesar Azpilicueta akitumia vizuri makosa ya Carl Jenkinson aliyerudisha mpira mfupi kwa kipa wake, Lukasz Fabianski na kunaswa na mfungaji na kukwamisha mpira wavuni. 

Arsenal walicharuka mara baada yta kuruhusu bao hilo lakini waishindwa kupenya ngome ya Chelsea na kujikuta wanaenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo moja.

Wakiwa katika mipango ya kusawazisha bao hilo Arsenal walijikuta wanafungwa nao la pili kwa shuti kali la Juan Mata ambalo lilijaa moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa asijue nla kufanya.

Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, Manchester United waliishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya Norwich City cha mabao 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 

Mabao ya Manchester yalifungwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’ mawili, Fabio na Phil Jones na kuwafanya timu hiyo kutinga hatia hiyo kwa ushindi mnono.

West Ham United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley wafungaji wakiwa Matt Taylor kwa penalti na Jack Collison, nao Stoke City walivuka hatua hiyo baada ya kuiondosha Birmingham City kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 4-4 katika dakika 120. 



Read more
Jumanne, 29 Oktoba 2013
YANGA NI MWENDO WA TATU TATU, YAIVUTA SIMBA CHINI, MBEYA CITY MWENDO MDUNDO

TIMU ya Yanga imeendeleza wimbi la ushindi wa mabao matatu baada ya leo kuitandika Mgambo Shooting mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga kushinda mabao matatu dhidi ya Rhino Rangers na leo Mgambo, huku ikishinda tatu dhidi ya Simba lakini wakafanikiwa kusawazisha.

Yanga ambao walikuwa uwanjani bila ya nyota wake, Haruna Niyonzima, walipata bao la kwanz kupitia kwa beki wake kiraka, Mbuyu Twite dakika ya 32 kwa shuti kali ya faulo kufanya timu yake kwenda mapumziko wakiwa mbele. 

Dakika 52 Yanga waliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Hamis Kiiza na kufunga bao lake na nane na kuwa sawa na kinara wa mabao Amisi Tambwe wa Simba, baada ya beki wa kipa wa Mgambo, Godson Mmasa kumwangusha mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.

Kavumbagu alishindilia msumali wa tatu kwa Mgambo kwa shuti kali lililomshinda kipa Mmasa na kutinga wavuni na kufanya Yanga kupata ushindi huo wa mabao matatu kwa mechi mbili mfululizo. 

Kwa matokeo hayo Yanga wamepanda hadi nafasi ya tatu na kuiacha Simba nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 22 wakiwa nyuma ya Mbeya City na Azam ambao wote wanapointi 23 huku wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Mbeya City nao wameitandika ndugu zao wa Prisons kwa mabao 2-0, shukrani kwa mabao ya Peter Mapunda dakika ya 67 na Deogratius Julius dakika ya 79.

Katika mchezo mwingine leo Rhino Rangers waliutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, mfungaji akiwa Abbas Mohamed dakika ya 71.

Read more
Jumatatu, 28 Oktoba 2013
IVO MAPUNDA ARUDISHWA TAIFA STARS, KIPIMO CHA KWANZA NOV 13

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya pili (Future Young Taifa Stars) kitakachoingia kambini Novemba 9 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kim kwenye kikosi hicho ambacho hukitumia kuangalia uwezo wa wachezaji kabla ya kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Kikosi hicho kamili ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars kinaundwa na; makipa Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).

Mabeki ni David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Himid Mao (Azam), Issa Rashid (Simba), Ismail Gambo (Azam), John Kabanda (Mbeya City), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Said Moradi (Azam) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Farid Mussa (Azam), Haruni Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga), William Lucian (Simba).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya (Mbeya City) na Paul Nonga (Mbeya City).

Kim amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager chenyewe kitaingia kambini Novemba 12 jijini Dar es Salaam ambapo siku inayofuata ndipo kitakapocheza mechi na Future Young Taifa Stars.

Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa wakati Taifa Stars itaondoka Novemba 14 mwaka huu kwenda Arusha ambapo itaweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).

Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).


Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
Read more
YANGA KUIPIKU SIMBA KESHO? KUVAANA NA MGAMBO TAIFA

LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha  raundi ya kumi na moja kesho (Oktoba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.


Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Read more
MCHEZAJI WA TIMU YA SAFARI POOL TAIFA, PATRICK NYANGUSI AMEIBUKA BINGWA WA AFRIKA (SINGLES)

Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi (kushoto) akiwa na mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini kabla ya kuanza mchezo wa fainali uliofanyika jijini Blantyre nchini Malawi mwishoni mwa wiki.

 Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.


Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.

 Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.





Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki

Mgeni rasmi, Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto) akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki. 
 
Mabingwa wa Afrika  wa mchezo wa pool wakiwa katika picha nya pamoja. Kutoka kushoto ni Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick Nyangusi,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki. 



Bingwa wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki.
Read more
 AZAM YAVUNJA MWIKO WA SIMBA, YAILAMBISHA 2-1

KIKOSI cha Simba leo imeonja uchungu wa kufungwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ambayo huu ndiyo mchezo wao wa kwanza kupoteza tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, bado ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji, Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya 13 akimalizia kazi safi ya Zahor Pazi aliyeitoka ngome ya Azam na kupiga krosi fupi iliyomkuta mfungaji.


Azam waliendelea kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 45 akimalizia krosi safi ya Erasto Nyoni na kufanya timu zote kwenye mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa bao 1-1.  

Kipindi cha pili mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa lakini Kipre aliizamisha jahazi la Simba baada ya kufunga bao la pili dakika ya 73 baada ya kufanya kazi kubwa ya kupangua ngome ya Simba na kumhadaa kipa, Abel Dhaira na mpira kujaa wavuni.

Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni mara baada ya mchezo huo alisema amekubali matokeo hayo na kilisababisha ni kutokuwa na wachezaji wake nyota lakini makosa yaliyofanywa na wachezaji wake ndiyo yaliyosbabisha kupoteza mchezo huo.
 Simba: Abel Dhaira, William Lucian, Issa Rashid, Hassan Khatib, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betrum Mombeki, Zahor Pazi/ Sino Augustino na Amri Kiemba/ Edward Christopha.

Azam FC: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Wazir Salum, Aggrey Morris. Said Morad/ David Mwantika, Boluo Kipre, Salum Aboubakary, Humphrey Mieno/ Khamis Mcha, John Bocco, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga.




   
Read more
CHRIS BROWN AMVUNJA MTU PUA BAADA YA KUMTWANGA NGUMI

MWANAMUZIKI Chris Brown bado anaendelea kuvunja sheria za huko Marekani. Sources mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya uhakika huko zinasema kwamba Chris amekamatwa pamoja na bodygurd wake baada ya Chris mwenyewe kumpiga ngumi ya uso na kumvunja pua jamaa mmoja waliyekutana kwenye hotel.

Habari juu ya tukio hilo linasema kwamba wasichana wawili walikuwa wanapiga picha na Chris Brown na wakati huohuo jamaa huyo alijaribu kwenda kwa nyuma na kuharibu picha hiyo (Photoboom). Chris Brown alivyomuona ndio hasira zake zikamfanya amrushie ngumi ya uso na kumpata puani.

Watu wakaribu na Chris Brown wametoa habari tofauti juu ya tukio hili na kusema kwamba huyo jamaa alikuwa anajaribu kupanda tour bus la Chris Brown lakini alizuiwa. Jamaa huyoalitaka kupanda baada ya wasichana wengine kukataliwa sasa katika harakati za kuzuiwa asiingine ndio aliumia puani.


Read more
VETTEL HANA MPINZANI FORMULA ONE ‘LANGALANGA’, ATWAA UBINGWA 2013

DEREVA wa timu ya mbio za magari yaendayo kasi ya Formula One ‘Langalanga’ wa Redbull, Sebastiani Vettel amewadhihirishia mapenzi wa mashindano hayo kuwa hana mpinzani kwa sasa baada ya kutawazwa kuwa bingwa wa mbio hizo mwaka huu huku kukiwa bado mashindano hayo yajamalizika.

Vettel ametangazwa kuwa bingwa wa Langalanga 2013 jana usiku baada ya kushinda mbio zilizofanyika nchini India huku kukiwa badoi kumebakia na mashindano matatu ya mbio hizo.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 26 aliendesha gari lake bila matatizo yoyote kufanikisha ushindi wake wa mara ya sita mfululizo msimu huu na kujitokeza kuwa dereva wa nne katika historia ya mashindano haya kufanya hivyo.

Baada ya mbio hizo Vettel alisema, nashindwa hata kusimulia, nimevuka msitari wa kumaliza mbio nikapoteza kauli. Najitahidi kutafuta maneno lakini nashindwa. Ni msimu mzuri kwake, timu yake  ina furaha kubwa sana.

Ushindi huu ni wa sita mfululizo na wa kumi kwa ujumla wa msimu mzuri kwake ambao unaweza kumsogeza karibu na rekodi inayoshikiliwa na Schumacher aliyeshinda jumla ya mbio 13 katika msimu mmoja.

Licha ya uwezo wake wa kushinda hata hivyo, Vettel ameshindwa kuwa na mvuto katika ushindi wake. Mfano ni ushindi wake huko Ubelgigi, Uingereza, Canada na Singapore ambako alizomewa na kwenye medani ya India alisimulia na jinsi kuzomewa huko kulivyomuathiri.

Amesema kuwa nilizomewa ingawa sikufanya kosa lolote na hilo liliniudhi kiasi lakini majibu nimeyatoa kwa ushindi uwanjani.

Endapo Vettel atashinda mbio tatu zilizosalia huko Abu Dhabi, Marekani na Brazil atafikia pia ushindi wa mara tisa wa Albert ASCARI wa mwaka 1952 na 1953.


Hata hivyo mpango mpya wa utaratibu utakaoanza mwaka 2014 kuendelea mbele ukihusisha mfumo mpya wa Ingini za magari pamoja na mfumo wa kuwezesha ingini ziongezewe nguvu --yanaweza kuzidisha ushindani wa mbio hizi.
Read more
MALINZI RAIS MPYA WA TFF, KARIA AWABWAGA MADEGA NA NASSIB

Tenga akimkabidhi mpira Malinzi kuashiria yeye ndiye kiongozi mpya mkuu wa soka nchini
JAMAL Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.  
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi kulia kuwa Rais mpya wa shirikisho.

Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.

Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.

Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.

Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James

 Anampa shada la maua ishara ya kumuachia madaraka

Kwaherini; Tenga akiwaaga Wajumbe

Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.

Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.


Anamkabidhi Katiba ya TFF

Eley Mbise amepata kura  51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
Kamati mpya ya Utendaji ya TFF

Habari na Picha kwa Hisani ya Bin Zubeiry
Read more