Open top menu
Jumatatu, 30 Septemba 2013
PICHA ZA FAINALI YA KIGOLI 2013 JANA TRAVERTINE

 Washiriki wa shindano la Kigoli 2013 wakishambulia jukwaa mmoja mmoja katika fainali hizo zilizofanyika jana katika Hoteli ya Travertine jana usiku





 Mwaandaji wa shindano la Kigoli 2013 na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Maimatha wa Jesse akicheza wimbo wa My No One wa Diamond katika fainali hizo

 Msanii wa kizazi kipya, Dyna alikuwepo kutumbuiza katika fainali hizo, hapa akiimba sambamba na shabiki wake




Waimbaji wa Jahazi wakiburudisha 
Kundi la muziki wa dansi la Kalunde Band walikuwepo kusindikiza fainali hizo
Kivazi hiki kilichovaliwa na mmoja wa washiriki wa shindano hilo kilizua balaa ukumbini
Mzee Yusuph akiwapagawisha mashabiki
 Mkoko ulioshindaniwa aina ya Nissani March wenye thamani ya Sh 9 milioni




Read more
Alhamisi, 26 Septemba 2013
 AIRTEL YAJITOSA ROCK CITY MARATHON


Meneja Matukio wa Capital Plus, Mathew Kasonta (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando na Ofisa Uhusiano CP, Geofrey Nangai.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando akionesha fomu za kujisajili kushiriki mbio hizo.  Kulia ni Meneja Matukio wa Capital Plus, Mathew Kasonta na Ofisa Uhusiano CP, Geofrey Nangai.


KAMPUNI ya Airtel ya Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa mara ya tano mfululizo imetangaza kudhamini mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zilizopangwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27, Oktoba 2013 ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya mchezo wa riadha nchini.

Airtel imekuwa mdhamini mkuu kwa upande wa mawasiliano katika mbiyo hizo, wakishirikiana na wadhaminiwa wengine kama NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications pamoja na Umoja Switch, ili kutoa fursa ya kuinua mchezo wa riadha inchini.

Akizungumza wakati wa tukio fupi lililofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema kampuni yake imejidhatiti kusaidia  shughuli mbali mbali za maendeleo ya jamii na mbio za Rock City Marathon pia ni fursa pekee ya kukuza vipaji katika michezo huo kwa ujumla.

“Kampuni ya Airtel Tanzania kwa mwaka wa tano mfululizo, leo hii tunatangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ikiwa ni sehemu ya jitihada zetu za kusaidia maendeleo ya michezo nchi nzima.

“Tunaamini kuwa mchango wetu utasaidia katika kuvumbua vipaji vipya vitakavyoshiriki si tu kwa mashindano ya kitaifa lakini pia na ya kimataifa,” alisema.

Mmbando aliongeza kuwa washiriki kwa mwaka huu wataweza kusajili moja kwa moja kupitia huduma ya kampuni yake ya Airtel Money kwa kutuma malipo yao kwa neno MARATHON na kuhifadhi ujumbe kwa ajili ya kuuonyesha wakati wa kuchukua fomu katika vituo mbali mbali.

Kwa upande wake mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta wakati wa tukio alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa na bora zaidi kwa kuleta pamoja washiriki kutoka ndani ya nje ya nchi.

 “Kwa mwaka huu tumeungana na kampuni ya Airtel lakini kupitia Airtel Money ili kutanua wigo wa ushiriki zaidi. Katika miaka iliyopita, watu wengi wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki au wakilazimika kusafiri umbali mkubwa kwenda kwenye vituo vichache tulivyoviandaa ili waweze kununua fomu za usajili, kwa kupitia Airtel Money zoezi hili litakuwa limerahisishwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Kasonta.

Kasonta aliongeza, “ukishamaliza zoezi hilo, utapokea ujumbe utakaouonyesha pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza.”

Alisema kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata fomu zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu, upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Kasonta alibainisha kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi).

Alisema kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.


Read more
 M 2 THE P AENDA KUSAKA UBANI NYUMBANI


BAADA ya kupata matatizo nchini Afrika Kusini, msanii wa kizazi kipya, Mgaza Pembe anayefahamika zaidi kama M 2 THE P, ameamua kwenda nyumbani kwao Mlandizi kusaka ubani kwa kufanya onyesho kwa wakazi wa mji huo.

M 2 THE P ambaye alikutwa na matatizo na msanii mwenzake, Albert Mangwea ambaye alifariki dunia, amefyatua kibao chake kipya alichokipa jina Masambe Wena (Twenzetu sasa) ambacho kimekuwa kinafanya vizuri katika radio na televisheni za hapa nchini.

Msanii huyo aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani kuwa ameamua kufanya onyesho hilo maalum kwa ndugu zake wa Mlandizi katika Ukumbi wa Super Night ikiwa sehemu ya shukrani kwa kumuomba wakati wa matatizo.

“Toka nimerudi na kufanya kazi yangu ya muziki nilikuwa sijawahi kuja nyumbani kufanya onyesho lolote,” alisema M 2 THE P. “Show hii ni maalumu kwa watu wangu wa Mlandizi kwa lengo la kuwapa shukrani kwa maombi yao.

“Nimefanya show nyingi nje ya kwetu katika Fiesta, nikaona kuna sababu ya kurudi nyumbani kushow love na ndugu zangu.”

Alisema kiingilio katika show hiyo kitakuwa Sh 3,000 kwa lengo la kumfanya kila mtu awe na uwezo wa kuingia na kupata burudani kutoka kwa msanii wao na wale watakaomsindikiza.

Wasanii ambao watamsindikiza M 2 THE P katika show hiyo ni Country Boy, Nyandu Tozi, Mirrow, Luteni Kalama, Isabela wa Scorpion Girls, Suma G, Shantiwa, Kionee, Ally Maowa na Punchiz Niggaz.


Read more
 KARAMA NYILAWILA KUZIPIGA OKTOBA 20


BONDIA wa Ngumi za Kulipwa nchini, Karama Nyilawila anatarajia kuvunja ukimya wa muda mrefu kwa kupanda ulingoni Oktoba 20 jijini Dar es Salaam kuvaana na Sado Philimon.

Nyilawila ambaye aliwahi kuwa bingwa wa mkanda wa WBF uzito wa middle baada ya kumpiga bondia wa Jamhuri ya Czech, Kreshnik Qato lakini alishindwa kuutetea mkanda huo hivyo kupotea katika medani ya masumbwi kwa kukosa mapromota.

Nyilawila anatarajia kuvaana na Sado katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala mpambano ulioandaliwa na Bigright Promotion chini ya Ibrahim Kamwe.

Kamwe aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani, maandalizi ya mapambano huo yanakwenda vizuri na wanatarajia kutakuwa na ushindani mkubwa kutokana na maamndalizi ya mabondia hao.

Read more