Open top menu
Ijumaa, 24 Januari 2014
VUMBI LIGI KUU KUANZA KESHO, YANGA ‘WAZEE WA UTURUKI’ KUWAVAA ASHANTI TAIFA

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.

Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.


Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.
Read more
Alhamisi, 23 Januari 2014
UFALME WA MAN UNITED WAZIDI KUPOTEA

UFAMLE wa klabu ya Manchester United umezidi kuporomoka baada ya kupokwa nafasi ya kwanza kuwa klabu tajiri duniani na nafasi hiyo sasa inashikiriwa na Real Madrid ya Hispania.

Manchester United ambayo sasa ipo katika msimu mbaya baada ya kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya England lakini sasa imepoteza heshima ya nje ya uwanja.

Klabu hiyo ambayo ilikuwa nafasi ya kwanza mwaka jana lakini sasa imetupwa mpaka nafasi ya nne, kwani nafasi tatu za juu zimechukuliwa na Madrid, Barcelona ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani.

Madrid imeshika nafasi hiyo baada ya kuingia zaidi ya euro 518 milioni katika msimu wa 2012/13, wakifuatiwa na Barcelona iliyoingia euro 482 milioni wakati Bayern inashika nafasi ya tatu ikiingiza euro 431.

Nafasi ya nne ipo Manchester United iliyoingia euro 423 na Paris Saint-Germain ‘PSG’ ya Ufaransa imeshika nafasi ya tano kwa kuingiza euro 398 milioni.


Read more
MOYES AMTOA KWA MKOPO ZAHA

KLABU ya Manchester United imemtoa kwa mkopo mshambuliaji wake kinda, Wilfried Zaha kwa timu ya Cardiff City ili apate muda mwingi wa kucheza.

Kinda huyo ambaye hakuwa na mahusaino mazuri na Kocha wake, David Moyes alionekana katika picha akiwasili kwenye hospitali ya Bridgewater iliyoko katika mji wa Manchester kwa lengo la kupima afya kabla ya kumalisha usajili huo wa mkopo.


Vyanzo vya karibu na mshambuliaji huyo walisema kuwa mpango huo unatarajiwa kukamilika haraka iwezekanavyo ili kutoa nafasi kwake kuongeza uwezo kabloa ya kurejea tena mikononi mwa Moyes.
Read more
HAZARD AICHOMOLEA PSG

WINGA wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard ameikataa ofa ya Paris Saint-Germain ‘PSG’ ya Ufaransa na badala yake ameweka kuwa ataendelea kuitumikia klabu yake.

Hazard ametajwa kuwa ni mmoja wa wachezaji wanaotakiwa na klabu ya PSG katika usajili wa dirisha dogo lakini nyota huyo amefunguka na kusema kuwa hayuko tayari kwa sasa kuihama Chelsea.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji anasema Chelsea ndiyo sehemu sahihi kwake kwa sasa kwani uwepo wake klabuni hapo kunampa nafasi zaidi ya kujiendeleza kisoka.


Read more
CHELSEA WATIBUA DILI LA LIVERPOOL

KLABU ya Chelsea inaweza kuharibu mipango ya Liverpool ya kumsajili winga wa FC Basel, Mohamed Salah baada ya kuweka mezani dau ya pauni 11 milioni ambazo ni zaidi ya kiasi kilichotengwa na Majogoo wa Anfield.

FC Basel walikuwa tayari kumuuza nyota huyo wenye umri wa miaka 21, kwa dau la pauni 10 milioni lakini Liverpool walikuwa tayari kutoa pauni 7 milioni.

Jose Mourinho amevutiwa na mchezaji huyo ambaye aliwafunga katika michezo yote miwili waliokutana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.


Pamoja na Salah kunukuliwa aakisema kuwa atafurahi zaidi kisaini kuichezea Liverpool lakini dau kubwa la Chelsea linaweza kuharibu mipango hiyo.
Read more
AMIN, MAKHIRIKHIRI KUMSINDIKIZA BANZA STONE JUMAMOSI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' Amin na kundi la Sanaa la Makhirikhiri wa bongo ni miongoni mwa burudani zitakazosindikiza onyesho maalumu la 'Usiku wa Banza Stone’  la bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Wazee wa Kizigo.

Onyesho hilo maalum kwa ajili ya kumtambulisha mtunzi na mwimbaji wake Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anayerejea upya jukwanii Jumamosi hii ndani ya Meeda Club Sinza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na tayari Banza ameanza mazoezi makali ya kufua sauti yake tayari kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi waliokuwa wame-mis sauti na tungo zake. 

Kwa muda wa miezi mitatu Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishia kushindwa kupanda jukwaani kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  bendi hiyo lakini akalazimika kupewa mapumziko ili aweze kufanya mazoezi na kula kwa mpangilio ili aweze kuimarisha afya yake.

Alisema, Amin na Makhirikhiri wa Bongo ni sehemu  tu ya burudani zitakazopamba 'usiku wa Banza Stone' kwani kutakuwa na vikundi vingine vya sanaa vitakavyonogesha onyesho ambapo mara baada ya onyesho hilo wataendelea kumtambulisha Banza katika kumbi mbalimbali za burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya ziara nyingine katika baadhi ya Mikoa.


Read more
FALCAO KULIKOSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Mshambuliaji wa timu ya Monaco na Colombia, Radamel Falcao atazikosa fainali la Kombe la Dunia kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Klabu ya Monaco imethibitisha kuwa mshambuliaji wao atakuwa nje kwa miezi sita, daktari wa timu hiyo, Jose Carlos Norona amethibitisha kuwa nyota huyo atazikosa fainali hizo ziutakazofanyika nchini Brazil mwezi wa Mei mwaka huu.


Read more
Alhamisi, 9 Januari 2014
BANZASTONE KUTAMBULISHWA JANUARI 25

MTUNZI na mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo 'Next Level Wazee wa Kizigo' Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anatarajiwa kutambulishwa rasmi kurejea kwake upya jukwaan Januari 25 mwaka huu katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Meeda Club Cnza jijini Dar es Salaam.

Kwa muda wa miezi miwili Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya hivi karibuni kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  Extra Bongo.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo Banza amepewa mapumziko maalumu ya wiki tatu kuimarisha afya yake na kufanya mazoezi tayari kujiandaa kurejea jukwaani kwa kishindo kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi waliokuwa waki -mis sauti na tungo zake.

“Tumeamua kumpa wiki tatu apumzike ambapo atazingatia kula vizuri, mazoezi binafsi sambamba na kupata muda wa kupumzika ili aweze kurudisha afya awe katika muonekano tofauti na sasa,” alisema.

Katika ziara ya Kanda ya Ziwa Banza alipata nafasi ya kuweza kuimba vipande vyake (mega mix) ingawa hakuweza kupewa nafasi ya kukaa muda mrefu stejini kutokana na afya kutoimarika vya kutosha.


Alisema, Extra Bongo kwa kutambua thamani ya afya ya mwanamuziki wake imeamua kumpumzisha Banza ili kujipanga kuwapa ujio wake mpya aliowaandalia wadau wa muziki wa dansi.
Read more
Ijumaa, 3 Januari 2014
  GUMBO, KINJE WAPATA DILI SHELISHELI

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.

Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.


TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
Read more
ISRAEL NKONGO, MBAGA WAULA FIFA

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.

Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.


Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.
Read more