KLABU ya Manchester United imemtoa kwa mkopo
mshambuliaji wake kinda, Wilfried Zaha kwa timu ya Cardiff City ili apate muda
mwingi wa kucheza.
Kinda huyo ambaye hakuwa na mahusaino mazuri na Kocha
wake, David Moyes alionekana katika picha akiwasili kwenye hospitali ya
Bridgewater iliyoko katika mji wa Manchester kwa lengo la kupima afya kabla ya
kumalisha usajili huo wa mkopo.
Vyanzo vya karibu na mshambuliaji huyo walisema kuwa
mpango huo unatarajiwa kukamilika haraka iwezekanavyo ili kutoa nafasi kwake
kuongeza uwezo kabloa ya kurejea tena mikononi mwa Moyes.
0 comments