Open top menu
Alhamisi, 23 Januari 2014
CHELSEA WATIBUA DILI LA LIVERPOOL

KLABU ya Chelsea inaweza kuharibu mipango ya Liverpool ya kumsajili winga wa FC Basel, Mohamed Salah baada ya kuweka mezani dau ya pauni 11 milioni ambazo ni zaidi ya kiasi kilichotengwa na Majogoo wa Anfield.

FC Basel walikuwa tayari kumuuza nyota huyo wenye umri wa miaka 21, kwa dau la pauni 10 milioni lakini Liverpool walikuwa tayari kutoa pauni 7 milioni.

Jose Mourinho amevutiwa na mchezaji huyo ambaye aliwafunga katika michezo yote miwili waliokutana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.


Pamoja na Salah kunukuliwa aakisema kuwa atafurahi zaidi kisaini kuichezea Liverpool lakini dau kubwa la Chelsea linaweza kuharibu mipango hiyo.
Read more
AMIN, MAKHIRIKHIRI KUMSINDIKIZA BANZA STONE JUMAMOSI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' Amin na kundi la Sanaa la Makhirikhiri wa bongo ni miongoni mwa burudani zitakazosindikiza onyesho maalumu la 'Usiku wa Banza Stone’  la bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Wazee wa Kizigo.

Onyesho hilo maalum kwa ajili ya kumtambulisha mtunzi na mwimbaji wake Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anayerejea upya jukwanii Jumamosi hii ndani ya Meeda Club Sinza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na tayari Banza ameanza mazoezi makali ya kufua sauti yake tayari kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi waliokuwa wame-mis sauti na tungo zake. 

Kwa muda wa miezi mitatu Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishia kushindwa kupanda jukwaani kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  bendi hiyo lakini akalazimika kupewa mapumziko ili aweze kufanya mazoezi na kula kwa mpangilio ili aweze kuimarisha afya yake.

Alisema, Amin na Makhirikhiri wa Bongo ni sehemu  tu ya burudani zitakazopamba 'usiku wa Banza Stone' kwani kutakuwa na vikundi vingine vya sanaa vitakavyonogesha onyesho ambapo mara baada ya onyesho hilo wataendelea kumtambulisha Banza katika kumbi mbalimbali za burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya ziara nyingine katika baadhi ya Mikoa.


Read more
FALCAO KULIKOSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Mshambuliaji wa timu ya Monaco na Colombia, Radamel Falcao atazikosa fainali la Kombe la Dunia kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Klabu ya Monaco imethibitisha kuwa mshambuliaji wao atakuwa nje kwa miezi sita, daktari wa timu hiyo, Jose Carlos Norona amethibitisha kuwa nyota huyo atazikosa fainali hizo ziutakazofanyika nchini Brazil mwezi wa Mei mwaka huu.


Read more
Alhamisi, 9 Januari 2014
BANZASTONE KUTAMBULISHWA JANUARI 25

MTUNZI na mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo 'Next Level Wazee wa Kizigo' Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anatarajiwa kutambulishwa rasmi kurejea kwake upya jukwaan Januari 25 mwaka huu katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Meeda Club Cnza jijini Dar es Salaam.

Kwa muda wa miezi miwili Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya hivi karibuni kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  Extra Bongo.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo Banza amepewa mapumziko maalumu ya wiki tatu kuimarisha afya yake na kufanya mazoezi tayari kujiandaa kurejea jukwaani kwa kishindo kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi waliokuwa waki -mis sauti na tungo zake.

“Tumeamua kumpa wiki tatu apumzike ambapo atazingatia kula vizuri, mazoezi binafsi sambamba na kupata muda wa kupumzika ili aweze kurudisha afya awe katika muonekano tofauti na sasa,” alisema.

Katika ziara ya Kanda ya Ziwa Banza alipata nafasi ya kuweza kuimba vipande vyake (mega mix) ingawa hakuweza kupewa nafasi ya kukaa muda mrefu stejini kutokana na afya kutoimarika vya kutosha.


Alisema, Extra Bongo kwa kutambua thamani ya afya ya mwanamuziki wake imeamua kumpumzisha Banza ili kujipanga kuwapa ujio wake mpya aliowaandalia wadau wa muziki wa dansi.
Read more
Ijumaa, 3 Januari 2014
  GUMBO, KINJE WAPATA DILI SHELISHELI

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.

Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.


TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
Read more
ISRAEL NKONGO, MBAGA WAULA FIFA

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.

Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.


Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.
Read more
Jumatano, 1 Januari 2014
 ARSENAL YARUDI KILELENI ENGLAND, YAIBAMIZA CARDIFF CITY 2-0, LIVERPOOL, CHELSEA ZAUA

VINARA wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wamerudi katika nafasi yao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cardiff City uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.

Arsenal imeipiga kikumbo Manchester City ambao walikaa kileleni kwa saa moja baada ya kufikisha pointi 45 na kuwaacha City wakiwa na pointi 44.

Washika Bunduki hao wa London ilibidi wasubiri hadi dakika ya 88 baada ya mshambuliaji wake, Nicklas Bendtner kuwamisha mpira wavuni lakini dakika mbili baadaye Theo Walcott aliongeza bao la pili. 

Katika mchezo mwingine uliochezwa leo, Liverpool nao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City na kuwafanya kuchuka hadi nafasi ya nne kutoka nafasi ya tano, baada ya kufikisha pointi 39.

 Mabao ya Liverpool yamefungwa na Daniel Agger dakika ya 36 wakati bao la pili liliwekwa kimiani na Luis Suarez dakika ya 50 ya mchezo huo. 

Mabao ya Fernando Torres, Willian na Oscar yaliiwezesha timu ya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Southamptom katika mchezo uliochezwa mapema leo.


Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa mapema leo, Crystal Palace walitoshana nguvu na Norwich City baada ya kutoka sare ya mabao 1-1, Fulham leo imezinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United na Stoke City wamegawana pointi ya Everton kwa kutoka sare ya mabao 1-1, West Brom wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.


Read more
BREAKING NEWS: FID Q AWAGOMEA CLOUDS, ASHUKA JUKWAANI MWENBEYANGA

MWANAMUZIKI wa Hip Hop nchini, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amewagomea Madj wa Clouds na kuacha kuimba na kushusha jukwaani baada ya madj kushindwa kumpigia ala za muziki ‘beat’ na badala yake kupiga wimbo kamili.

Fid Q alionyesha ukomavu leo katika tamasha ya kusherehekea miaka 14 ya kituo cha redio cha Clouds baada ya kumwambia Dj Zero kupiga beat ya wimbo wake lakini dja huyo hakufanya hivyo na badala yake akaweka mic chini ya kushuka jukwaani.


Wasanii wote waliopanda katika tamasha hilo lililoandaliwa na Clouds redio walikuwa wakiimba nyimboa zao kamili kwa kurudia maneno yao yaliyorekodiwa kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa Fid Q.
Read more
 MAN CITY WAISHUSHA ARSENAL KILELENI, YAIPIGA SWANSEA 3-2

TIMU ya Manchester City imefanikiwa kuishusha kileleni Arsenal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Swansea katika mchezo mgumu uliomalizika muda mfupi uliopita.

Man City imekaa kileleni baada ya kujikusanyia pointi 44 na kuiacha kwa pointi mbili Arsenal ambao walimaliza mwaka uliopita wakiwa kileleni kwa pointi 42. 

Lakini Man City inaweza kusherehekea nafasi hiyo kwa muda mfupi kama Arsenal watashinda mchezo wao dhidi ya Cardiff City unaochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.

Mabao ya Man City yalifungwa na Fernandinho dakika ya 14, Yaya Toure dakika ya 58 na Aleksandar kolarov dakika ya 66 wakati mabao ya Wilfried Bony dakika ya 45 na 90.



Read more
MAN CITY YABANWA MBAVU NA SWANSEA, MAPUMZIKO SASA 1-1

WAKATI ikiwa ni mapumziko timu ya Manchester City wamebanwa mbavu ya Swansea na kulazimshwa sare ya mabao 1-1. Bao ya City limefungwa na Fernandinho dakika ya 14 wakati Swansea walisawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Wilfried Bony. 
Read more