Open top menu
Jumatano, 30 Oktoba 2013

TIMU ya Arsenal jana imeyaaga mashindano ya Capital One baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa hatua ya mtoano ya michuano hiyo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa vijana wa Jose Mourihno walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa beki wake wa kulia, Mhispania Cesar Azpilicueta akitumia vizuri makosa ya Carl Jenkinson aliyerudisha mpira mfupi kwa kipa wake, Lukasz Fabianski na kunaswa na mfungaji na kukwamisha mpira wavuni. 

Arsenal walicharuka mara baada yta kuruhusu bao hilo lakini waishindwa kupenya ngome ya Chelsea na kujikuta wanaenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo moja.

Wakiwa katika mipango ya kusawazisha bao hilo Arsenal walijikuta wanafungwa nao la pili kwa shuti kali la Juan Mata ambalo lilijaa moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa asijue nla kufanya.

Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, Manchester United waliishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya Norwich City cha mabao 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 

Mabao ya Manchester yalifungwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’ mawili, Fabio na Phil Jones na kuwafanya timu hiyo kutinga hatia hiyo kwa ushindi mnono.

West Ham United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley wafungaji wakiwa Matt Taylor kwa penalti na Jack Collison, nao Stoke City walivuka hatua hiyo baada ya kuiondosha Birmingham City kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 4-4 katika dakika 120. 



Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments