Open top menu
Jumanne, 1 Oktoba 2013
 CHALENJI KUTIMUA VUMBI NOV 27 NCHINI KENYA


MICHUANO ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Nchi wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu. Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.

Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab (Somalia), Tariq Atta (Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda).

Majina ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa miguu.

Read more
 BIFU LA PAPIC NA YANGA, MIKONONI KWA FIFA


SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewasilisha rasmi suala la madai ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya klabu hiyo katika Kamati ya Hadhi ya Wachezaji.

FIFA imesema imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya kupokea vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani pamoja na vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa akiidai klabu hiyo.

Kwa taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka pande hizo mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika. Zwanziger kitaaluma ni mwanasheria.

Papic aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko yake FIFA akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo ilikuwa haijamlipa dola 10,000 za Marekani.

Read more
SHAFFIH DAUDA, RUKAMBURA MWISHO KESHO TFF


WAKATI walalamikiwa waliofikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa wameshapokea uamuzi dhidi yao kwa maandishi, mwisho wa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili ni kesho (Oktoba 2 mwaka huu).

Walalamikiwa wote saba waliohudhuriwa mashauli dhidi yao; Kamwanga Tambwe, Nazarius Kilungeja, Omar Abdulkadir, Richard Rukambura, Riziki Majala, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao wamepokea uamuzi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Jessie Mnguto.

Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili, kwa ambao hawakuridhika na uamuzi huo wanatakiwa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili inayoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ndani ya siku tatu zinazomalizika kesho.

Rufani ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Kanuni ya 74 (1) na (2) ya Kanuni za Maadili, rufani zikionesha sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku tatu kwa njia ya posta (registered post or dispatch or courier service) kwa Sekretarieti.

Vilevile inatakiwa rufani inatakiwa kuambatanishwa risiti ya malipo ya ada ya rufani. Ada ya rufani ni sh. milioni moja.
Read more
 WOODS ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA


MKONGWE wa katika mchezo wa gofu, Tiger Woods ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo kwa mwaka 2013 ikiwa ni mara yake ya 11 kutwaa tuzo hiyo.

Wakati Woods akitawazwa kuwa mchezaji bora, Jordan Spieth naye amechaguliwa kuwa mchezaji bora kijana anayechipukia katika mchezo huo.

Woods, 37, amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kushinda mataji matano katika mashindano 11 aliyoshiriki ndani ya mwaka huu, wakati Spieth, 19, amekuwa mchezaji chipukizi mwenye mafanikio kwa mwaka huu.

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Woods kwani amefanikiwa kurudi katika namba moja baada ya kumbwaga aliyekuwa kileleni Rory McIlroy.

Read more
VICTORIA AZARENKA AVULIWA UBINGWA CHINA OPEN


BINGWA mtetezi wa michuano ya tenisi ya wazi ya China, Victoria Azarenka amevuliwa ubingwa wake katia raundi ya kwanza baada ya kutandikwa na mcheza tenisi namba 43 kwa ubora dunianio, Andrea Petkovic wa Ujerumani.

Mchezaji huyo ambaye anashikiria namba mbili kwa ubora duniani, alipoteza ubingwa wake baada ya kufungwa kwa 6-4 2-6 6-4 katika mechi ambayo ilicchukua masaa mawili na dakika 22.

Victoria ambaye alikuwa na kazi ngumu katika mchezo huo kuokoa mipira ya mpinzani lakini pia hakuwa vizuri kwani alipoteza mipiora 44 katika mchezo huo na kusababisha kupoteza ubingwa wake katika hatua ya mwanzo kabisa.

“Huu ulikuwa mchezo wangu mbaya sana na nimeonyesha kiwango cha chini sana,” alisema Victoria baada ya mchezo huo.

Read more