WAKATI walalamikiwa waliofikishwa kwenye Kamati ya
Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa wameshapokea
uamuzi dhidi yao kwa maandishi, mwisho wa kukata rufani Kamati ya Rufani ya
Maadili ni kesho (Oktoba 2 mwaka huu).
Walalamikiwa wote saba waliohudhuriwa mashauli dhidi
yao; Kamwanga Tambwe, Nazarius Kilungeja, Omar Abdulkadir, Richard Rukambura,
Riziki Majala, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao wamepokea uamuzi wa Kamati hiyo
inayoongozwa na Jessie Mnguto.
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili, kwa ambao
hawakuridhika na uamuzi huo wanatakiwa kukata rufani Kamati ya Rufani ya
Maadili inayoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ndani ya siku tatu
zinazomalizika kesho.
Rufani ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya
saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Kanuni ya 74 (1) na (2) ya Kanuni za
Maadili, rufani zikionesha sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwasilishwa
ndani ya siku tatu kwa njia ya posta (registered post or dispatch or courier
service) kwa Sekretarieti.
Vilevile inatakiwa rufani inatakiwa kuambatanishwa
risiti ya malipo ya ada ya rufani. Ada ya rufani ni sh. milioni moja.
0 comments