MICHUANO ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika
Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
Nchi wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa
kuthibitisha ushiriki wao kwa Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka
huu. Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya,
Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.
Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA
utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na
ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe
wa Kamati ya Utendaji.
Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian
wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab
(Somalia), Tariq Atta (Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda).
Majina ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa
katika Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa
yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa miguu.
0 comments