Open top menu
Jumamosi, 31 Agosti 2013
BREAKING NEWS: Cheka amtwanga Mmarekani kwa pointi


Nyota ya bondia wa Tanzania, Francis Cheka imezidi kung’ara baada ya kumtwanga kwa pointi bondia kutoka Marekani, Phill Williams katika mpambano wa raundi 12 wa kuwania mkanda wa dundia wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBO).

Cheka ambaye alionekana kutawala mpambano huo toka raundi ya kwanza alifalifanikiwa kumwangusha mpinzani wake lakini aliendelea na kumaliza hadi raundi ya mwisho.

Bondia huyo ambaye hana mpinzani hapa nchini amekabidhiwa mkanda wake WBO.
Read more
Ijumaa, 30 Agosti 2013
Kumbe Maugo alichungulia, apigwa kwa poindi na Mashali


Pamoja na bondia Mada Maugo kugoma kupanda ulingoni kwa muda lakini hakuepuka kipigo kutoka kwa mpinzani wake, Thomas Mashali baada ya kutwangwa kwa pointi.

Mpambano huo ambao ilikuwa wa raundi 10 kuwania mkanda wa Afrika  wa uzito wa feather ulikuwa na ushindani katika raundi zote lakini hadi kufika mwisho wa mpambano huo, Mashali ameibuka kidedea kwa pointi.

Mashali amekabidhiwa mkanda na bondia wa zamani wa uzito wa juu wa Marekani, Francois Botha hivyo kutawazwa rasmi kuwa bingwa wa mkanda huo.

Usitoke nyumbani endelea kupata kinachojili katika mapambano kati ya Francis Cheka na William kutoka Marekani.
Read more
BREAKING NEWS: Maugo agoma kupanda jukwaani Diamond, Botha aokoa


Tasnia ya ngumi nchini Tanzania jana iliingia aibu mbele ya bondia mkongwe Francois Botha kutoka Marekani, baada ya bondia Mada Maugo kutoka kupanda jukwaani kupambana na Fransic Mashali kwa zaidi ya nusu saa.

Maugo aligoma kupanda ulingoni kwa madai kuwa hajalipwa fedha zake kwa ajili ya mpambano huo wa raundi 10 wa kuwania mkanda wa Afrika wa uzito wa feather dhidi ya Mashali.

Pambano hilo ambalo lilikuwa la utangulizi kabla ya lile ya Fransic Cheka wa Tanzania na William wa Marekani, lilisubiri kwa muda kutokana na kisanga hicho hadi pale bondia wa zamani wa uzito wa juu, Botha kuingilia kati na kumwomba Maugo apande ulingoni na atamlipa yeye fedha zake.

Endelea kubaki ndani ya nyumba ili uendelee kupata kinachojiri huko Diamond
Read more