Ivanovic (kulia) akionekana kumpiga kiwiko Benteke
BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic, amenusurika
kuingia katika adhabu ya Chama cha Soka England (FA) licha ya kuonekana kumpiga
kiwiko mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke, katika mchezo wa jana
usiku.
Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert, alikuwa mwenye
hasira kwa mwamuzi wa mchezo huo, Kevin Friend, aliyeamua kutompa kadi nyekundu
beki huyo wa kimataifa wa Serbia kwa tukio hilo, sekunde chache kabla ya
kuifungia Chelsea bao la ushindi.
Lakini kwa sababu Friend alimuonesha kadi ya njano
beki huyo, na aliliona tukio hilo la kupigwa kwa kiwiko Benteke, FA haitachukua
hatua yoyote.
Sheria za FA zilibadilishwa katika majira ya joto
kwa tukio kama hilo msimu uliopita, ambapo mchezaji wa Wigan, Callum McManaman,
ambaye alikimbia adhabu kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Newcastle, Massadio
Haidara.
Hata hivyo, sheria hiyo inasema kuwa FA wangeweza
kumchukulia hatua zaidi mchezaji huyo kama mwamuzi aneandikakatika ripoti yake
kuwa hakuliona tukio hilo.
0 comments