MSANII nyota wa filamu na muziki, Snura Mushi
'Snura' amevunja ukimya na kuwaambia wanaume wakware kuwa hatumii kiuno chake
kutafuta mabwana bali anakitumia kusaka pesa.
Snura amelazimika kufungua kwa style hiyo kutokana
na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume ambao wanapagawa na jinsi anavyomudu
kuzungusha kiuno jukwaani kwani pamoja na kudata lakini hawataweza kukiona 'live'.
Msanii huyo anayetamba na nyimbo zake za Majanga na Nimevurugwa, aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani kuwa
kuna wanaume wengi wanadhani anapokatika viuno kwenye show zake basi anatafuta
wanaume huku wakisahau kuwa ile ni kazi inayompa kula.
Alisema inawezekana wanaume wakawa wanakitamani na
wanaamini kuwa anakitumia kwa ajili ya mapenzi na kuwadatisha wenye hela,
ingawa ndani ya nafsi yake anajua nini anachokifanya na hayuko kama mastaa
wengine wanaishi mjini kwa nguvu za wanaume.
"Mimi sipo kama mastaa wengine, natumia kiuno
changu kusaka pesa na si wanaume,”
alisema Snura. “Kiuno change ndicho kinanipa kula na ndiyo maana kila siku
manjonjo yanaongezeka.”
0 comments