Open top menu
Alhamisi, 26 Septemba 2013
LIGI KUU TANZANIA BARA KUMECHAFUKA


IDADI ya kadi zilizotolewa katika michezo saba iliyochezwa wiki iliyopita inaonyesha kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa haina nidhamu.

Katika michezo saba iliyochezwa kwa kukutanisha timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo jumla ya kadi 22 zimetolewa huku zote zikiwa za njano.

Pamoja na kadi hizo kuwa za njano lakini haitoshi kuoinyesha kuwa katika michezo hiyo madhambi mengi yametendeka kiasi cvha kuwafanya waamuzi kuwaonya wachezaji kwa kadi hizo za njano.

Katika ripoti hiyo ya wiki iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaonyesha kuwa jumla ya michezo saba imechezwa mwishoni mwa wiki iliyopita Septemba 21 na 22 katika viwanja saba.

Jumla mabao yaliyofungwa katika michezo hiyo ni 18 yamefgungwa katika michezo yote saba ikiwa na idadi hiyo ya kadi zilizotolewa na waamuzi.

Mbali na kadi hizo zilizotolewa katika michezo hiyop saba lakini hadi sasa toka ligi hiyo ianze jumla ya kadi 116 zimetolewa huku nyekundu zikiwa tano na kadi za njano 111.
Read more
Jumatano, 25 Septemba 2013
RODGERS: SIHOFII KUMPANGA SUAREZ LEO




























KOCHA Brendan Rodgers ameliambia gazeti la Guardian la England kuwa hahofii kumtumia Luis Suarez katika kikosi cha Liverpool kinachokipiga na Manchester United leo katika mchezo wa kwanza wa Capital One Cup.

Suarez yuko katika listi ya Rodgers tena baada ya kufungiwa michezo 10, huku akiukosa mchezo wa kichapo cha bao 1-0 walichokipta mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Southampton, kifungo alichokipata baada ya kumng'ata kwa makusudi beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, msimu uliopita.

Na anatarajiwa kurudi katika mchezo huo unaopigwa leo kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati mchezaji huyo pia akikumbukwa kwa kufungiwa michezo nane kwa kumtolea lugha ya kibaguzi beki wa United, Patrice Evra 2011.

Rodgers anaamini kuwa Suarez atakuwa tayari kupokea mapokezi mabaya Old Trafford. Na alisema: "Sihofii chochote juu ya kumpanga Luis. Tangu nimekuwa hapa sikuwahi kukutana na kitu kama hicho. Kuna historia katika michezo hii lakini sielekezi akili yangu huko.

"Luis ni mchezaji mwenye jina kubwa. Na ni mmoja kati ya wachezaji wakubwa wenye matukio ambaye nimewahi kukutana naye katika maisha yangu. Sidhani kama mapokezi yatamchanganya.

"Ni mpiganaji na malengo yake ya kufanikiwa yapo kwa ajili ya kila mmoja kumuona. Tunafurahikuona kuwa amerudi kikosini. Najua hata wachezaji wana furaha kurudi kwa mchezaji huyu uwanjani kutokana na ubora wake."

Rodgers aliongeza: "Sidhani kama atakuwa katika ulinzi mkubwa kama ambavyo imekuwa katika michezo iliyopita. Luis ni aina hiyo ya mchezaji. Siku zote huzungumza anapochezewa vibaya. Kazi anayofanya anapokuwa ndani na karibu na eneo la hatari huwafanya mabeki kuwa katika wakati mgumu.

"Ni sehemu ya mchezo na unatakiwa kuendana nayo. Nafikiri huu ni mchezo mzuri kwetu baada ya kutoka vichwa chgini katika mchezo uliopita dhidi ya Southampton. Luis atakuwa sehemu ya mchezo huu.

"Nina uhakika kuwa wakati Luis atakapojua kuwa ni sehemu ya mchezo huu, itamshitua na kumfanya kuwa tayari kwa kutetea timu yake. Unaweza kuona kwamba huu ni mchezo mzuri kwake kwa ajili ya ujio mpya baada ya adhabu."
Read more
Jumanne, 24 Septemba 2013
WASANII MMESIKIA MANENO YA SKYNER?


 MREMBO anayetikisa kwenye tasnia ya filamu Bongo, Skyner Ally Seif anayependa ukimwita 'Skyner', amewapasha wasanii wenzake wasijidanganye na majina waliyokuwa kuwa nayo kwenye movie na kuamini kuwa wanaweza kufanya vizuri kwenye siasa.

Skyner ambaye anafanya vizuri katika tasnia hiyo kwa sasa amesema kuwa kwa upande wake hafikirii kujiingiza kwenye siasa kama wanavyofanya wasanii wengine wa filamu na muziki kwa sasa kwani anaamini kuwa mambo hayo siyo rahisi kama wengine wanavyofikiria.
Msanii huyo aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye siasa wakiamini kuwa kuna fedha nyingi na wanasahau kuwa siasa inahitaji kuwa na moyo wa kujitolea na kuwatumikia wananchi kitu ambacho anaamini wasanii wengi hawana moyo huo.

Alisema kuna kazi nyingi za kufanya na siyo siasa pekee, hivyo anaamini kwa upande wake sanaa ni changua lake kubwa ambalo linaweza kuinua maisha yake na kumpeleka mbali zaidi.

"Binafsi sina mpango kabisa wa kuingia kwenye siasa. Nawaomba wasanii wanaotaka kuingia kwenye siasa kwa lengo la kupata fedha za haraka, waachane na mipango hiyo kwani wananchi wanahitaji mtu wa kuwasimamia shida zao,” alisema Skyner.
Read more
BALOTELLI ATUPWA JELA ITALIA



Mario Balotelli alizuia na wachezaji wenzake asimfuate mwamuzi mara baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli

KLABU ya AC Milan itasafiri kwenda kuivaa timu ya Juventus mapema mwezi ujao bila ya mshambuliaji wake, Mario Balotelli baada ya kufungiwa mechi tatu kutokana na kufanya vurugu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mshambuliaji huyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo huo ambao walilala kwa mabao 2-1, Balotelli hakukubaliana na kadi hiyo na kuanza kumzonga mwamuzi.

Chama cha soka nchini Italia imemfungia michezo mitatu kutokana na kitendo chake cha kushambulia mwamuzi hivyo ataikosa michezo mitatu ikiwemo ule wa Juventus pamoja na Bologna na Sampdoria.

"Adhabu hiyo imetolewa kwa Balotelii kutokana na vitendo vyake vya kukwaruzana na wachezaji wa timu pinzani, mwamuzi wa akiba pamoja na kutokukubaliana na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo,” alisema mmoja wa maafisa wa chama hicho akifafanua adhabu  hiyo.


 Faulo iliyosababisha Balotelli kupewa kadi ya pili ya njano na kisha nyekundu
Read more
 DI MATTEO AITWA KUINOA SUNDERLAND


KOCHA wa zamani wa Chelsea, Roberto de Matteo amependekezwa kuwa chaguo la kwanza kuziba nafasi iliyoachwa na Paolo Di Canio kuiongoza klabu ya Sunderland.

Taarifa zinasema kuwa Mkurugenzi wake Black Cats amekuwa na mipango ya kumshawishi Di Matteo kujiunga na timu yake kuziba pengo la Di Canio na mazungumzo yao yanatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Kama De Matteo atakubaliana na Sunderland ataanza kazi mapema iwezekanavyo kabla ya mchezo wao dhidi ya Manchester United utakaochezwa Oktoba 5 mwaka huu.

Makocha wengine ambao wanawaniwa na Black Cats ni pamoja na Gus Poyet na Tony Pulis lakini hao ni cxhaguao la pili kama mambo yatakuwa magumu kwa Di Matteo ambaye ni chaguo la kwanza la uongozi wa klabu hiyo.

Di Matteo amekuwa nje ya uwanja wa uwanja toka Novemba mwaka jana baada ya kutimuliwa na klabu ya Chelsea baada ya kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Komnbe la FA katika miezi nane aliyoitumikia klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Read more
AIRTEL RAISING STAR KUPONGEZWA KEMPINSKI LEO


TIMU ya mpira wa miguu ya wasichana ya Airtel Raising Stars (ARS) ya Tanzania imeandaliwa hafla ya kuipongeza kwa kunyakua ubingwa katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.

Hafla hiyo ya kuipongeza pamoja na kupata chakula cha mchana itafanyika leo (Septemba 24 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na kuongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

Timu hiyo iliyorejea nchini jana usiku katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo iliifunga Kenya. Kwa upande wa wavulana, timu hiyo ilitolewa na Zambia katika hatua ya nusu fainali.

Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia.

Kombaini ya timu hizo zilizokuwa chini ya makocha Rogasian Kaijage na Abel Mtweve iliundwa baada ya mashindano ya Airtel Raising Stars yaliyohusisha wasichana na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 17 na kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Septemba mwaka huu.

Read more