Mario Balotelli alizuia na wachezaji wenzake asimfuate mwamuzi mara baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli
KLABU ya AC Milan itasafiri kwenda kuivaa timu ya
Juventus mapema mwezi ujao bila ya mshambuliaji wake, Mario Balotelli baada ya
kufungiwa mechi tatu kutokana na kufanya vurugu baada ya kutolewa kwa kadi
nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli uliochezwa mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mshambuliaji huyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada
ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo huo ambao walilala kwa mabao 2-1,
Balotelli hakukubaliana na kadi hiyo na kuanza kumzonga mwamuzi.
Chama cha soka nchini Italia imemfungia michezo
mitatu kutokana na kitendo chake cha kushambulia mwamuzi hivyo ataikosa michezo
mitatu ikiwemo ule wa Juventus pamoja na Bologna na Sampdoria.
"Adhabu hiyo imetolewa kwa Balotelii kutokana
na vitendo vyake vya kukwaruzana na wachezaji wa timu pinzani, mwamuzi wa akiba
pamoja na kutokukubaliana na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo,” alisema mmoja
wa maafisa wa chama hicho akifafanua adhabu
hiyo.
Faulo iliyosababisha Balotelli kupewa kadi ya pili ya njano na kisha nyekundu
0 comments