KOCHA wa zamani wa Chelsea, Roberto de Matteo
amependekezwa kuwa chaguo la kwanza kuziba nafasi iliyoachwa na Paolo Di Canio
kuiongoza klabu ya Sunderland.
Taarifa zinasema kuwa Mkurugenzi wake Black Cats amekuwa
na mipango ya kumshawishi Di Matteo kujiunga na timu yake kuziba pengo la Di
Canio na mazungumzo yao yanatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
Kama De Matteo atakubaliana na Sunderland ataanza
kazi mapema iwezekanavyo kabla ya mchezo wao dhidi ya Manchester United
utakaochezwa Oktoba 5 mwaka huu.
Makocha wengine ambao wanawaniwa na Black Cats ni
pamoja na Gus Poyet na Tony Pulis lakini hao ni cxhaguao la pili kama mambo
yatakuwa magumu kwa Di Matteo ambaye ni chaguo la kwanza la uongozi wa klabu
hiyo.
Di Matteo amekuwa nje ya uwanja wa uwanja toka
Novemba mwaka jana baada ya kutimuliwa na klabu ya Chelsea baada ya kuipa
ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Komnbe la FA katika miezi nane
aliyoitumikia klabu hiyo ya Stamford Bridge.
0 comments