TIMU ya mpira wa miguu ya wasichana ya Airtel
Raising Stars (ARS) ya Tanzania imeandaliwa hafla ya kuipongeza kwa kunyakua
ubingwa katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.
Hafla hiyo ya kuipongeza pamoja na kupata chakula
cha mchana itafanyika leo (Septemba 24 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hoteli ya
Kilimanjaro Kempinski na kuongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
Timu hiyo iliyorejea nchini jana usiku katika mchezo
wa fainali ya mashindano hayo iliifunga Kenya. Kwa upande wa wavulana, timu
hiyo ilitolewa na Zambia katika hatua ya nusu fainali.
Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka nchi za
Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC), Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na
Zambia.
Kombaini ya timu hizo zilizokuwa chini ya makocha
Rogasian Kaijage na Abel Mtweve iliundwa baada ya mashindano ya Airtel Raising
Stars yaliyohusisha wasichana na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 17 na
kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Septemba mwaka huu.
0 comments