Open top menu
Jumapili, 27 Oktoba 2013
WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA 'STOP' KURIPOTI UCHAGUZI WA TFF

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Juma Pinto (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Ukumbi wa Mikutano NSSF  'Water Front', mahala unapofanyika Uchaguzi mkuu wa Rais na viongozi wa Soka wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Waandishi wa Habari  wamezuiwa kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa NSSF Water Front.

Baada ya waandishi kuzuiwa, askari waliokuwa wakilinda usalama katika uchaguzi huo waliwataka waandishi kuondoka na kukaa mbali na ukumbi huo huku  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Juma Pinto, akiwataka waandishi kususia kuandika na kuripoti matokeo ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kutoandika taarifa za TFF.

Pinto alisema kitendo cha TFF kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni, kuwazuia waandishi kuripoti habari hizo ni cha udhalilishaji kwa kuwa waandishi ndio waliokuwa mstari wa mbele kuandika taarifa za uchaguzi huo tangu mchakato wake ulipoanza Februari mwaka huu.

Alisema mbali na kutoruhusiwa kuripoti uchaguzi huo, Mbwezeleni ametoa kauli ambazo si za kiungwana na kusahau kuwa waandishi ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwajuza Watanzania kuhusu uchaguzi huo kwa faida ya maendeleo ya soka la Tanzania.


 Kufuatia hali hiyo, iliwalazimu waandishi kukaa nje ya ukumbi huku wakiuliza kwa wajumbe kitu gani kinachoendelea ndani ya ukumbi.
Read more
*BREAKING NEEEWZ!!! BABA MZAZI WA WEMA SEPETU, BALOZI ISAAC SEPETU AFARIKI DUNIA

HABARI zilizotufikia hivi punde mtandao huu, zinasema kuwa, Baba Mzazi wa msanii wa Filam nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, Balozi Issac Abraham  Sepetu, amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.

Aidha imeelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.

Hadi umauti unamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Mtandao huu unaungana na waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Mahala Pema Peponi .

-Amen-


Read more
BARCELONA YAICHINJA MADRID, BALE ACHEMKA

MCHEZAJI ghali wa dunia, Gareth Bale jana alishindwa kutamba katika El Clasico yake ya kwanza toka alipotua katika klabu ya Real Madrid walipovaana na Barcelona ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Bale ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda akiwa anasumbuliwa matatizo ya mgongo, lakini jana alipangwa katika kikosi cha kwanza cha mchezo huo na Kocha wake, Carlo Ancelotti, lakini alishindwa kuonyesha kiwango kizuri na kuwaacha Barca watawale zaidi katika kipindi chote cha kwanza.

Ancelotti aliona mapungufu ya Bale na kulazimika kumtoa katika kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Kareem Benzema ambaye aliipa uhai timu yake lakini bado hawakuweza kutamba mbele ya Barca. 

Neymar ambaye naye ilikuwa Eli Clasico yake ya kwanza aling’ara katika mchezo huo na kuifungia timu ayke bao la kwanza dakika 19 wakati Sanchez aliongeza bao la pili akitumia uzembe wa kipwa wa Madrid, Diego Lopez baada ya kutoka mbele na kuliacha goli wazi.


Bao la Madrid lilifungwa na Jese Rodriguez katika dakika tatu za nyongeza na kuifanya timu yake kulala kwa mabao 2-1 katika mchezo huo.





Read more
ARSENAL YANG’ANG’ANIA KILELENI, MAN U YASHINDA, LIVER YAIFANYIA MBAYA WEST BROM

KIKOSI cha Arsene Wenger kimeendelea kujichimbia kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Crystal Palace mabao 2-0 uliochezwa jana.

Kwa ushindi huo Arsenal wamefikiwa pointi 22 wakifuatiwa na Liverpool wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 20 nao baada ya kushinda mchezo wao jana.

Mashabiki wa Arsenal walisubiri hadi kipindi cha pili ndipo wainuke na kuanza kushangilia bao lao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Mikel Arteta kwa njia ya penalti kabla ya Olivier Geroud kufunga kazi dakika chache kabla ya kipenga cha mwisho kulia.
Robin van Persie akiwa chini ya ulinzi wa wachezaji wa Stoke City
Katika mchezo mwingine Manchester United ilibuika na ushindi kwa mbinde dhidi ya Stoke City wakiwa nyumbani na kufanikiwa kushinda mchezo huo kwa mabao 3-2.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na ushindani mkubwa, Stoke ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Peter Crouch kabla ya Robin van Persie kusawazisha lakini mkwaju wa faulo wa Marko Arnautovic uliomshinda kipa wa Manchester United, David da Gea na kujaa wavuni na kuwafanya wenyeji waende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.

Mabao ya Wayne Rooney katika kipindi cha pili na Chicharito ambayo yote yalifungwa kwa kichwa ndiyo yaliyopeleka shangwe Old Trafford na kufanya Man Utd kuibuka na ushidni huo wa mabao 3-2.
Mshambuliaji wa Manchester United, Chicharito akifungao bao la tatu kwa kichwa 
Nao Liverpool jana walifanya mauaji baada ya kuikandamiza West Bromich mabao 4-1 huku Luis Suarez akionekana kurudi kwa kasi na kufunga hart-trick wakati bao linguine lilifungwa na Daniel Sturridge na bao la kufutia machozi la West Brom lilifungwa na James Morrison.

Matokeo mengine ya michezo iliyochezwa jana Everton ikichezea ugenini imeifunga Aston Villa mabao 2-0. Norwich imetoka suluhu na Cardiff City na Southampton ikaifunga Fulham mabao 2-0.


Read more
Ijumaa, 25 Oktoba 2013
JUMA PINTO ATOA SIRI YA KINACHOMPELEKA TFF

MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Juma Pinto amefunguka na kueleza sera na mikakati yake atakapoingia kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Uchaguzi huo wa TFF unatarajia kufanyika Jumapili ya Oktoba 27, Pinto anagombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda ya Pwani na Morogoro.

Pinto aliuambia mtandao huu kuwa, nimeamua kugombea nafasi hiyo ili  kuleta mabadiliko ya kweli na kuleta fikra endelevu katika soka la Tanzania.

Naamini kabisa nikichaguliwa katika nafasi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutaleta mafanikio zaidi na hususani kupokea kijiti kwa viongozi wenzetu waliotangulia ambao wameweka mfumo mzuri wa utawala bora ndani ya shirikisho.

Ili mafanikio yaweze kupatikane ni lazima tuweke mpango endelevu kwa kuwekeza zaidi katika soka la vijana, kuandaa kozi ,warsha na makongamano yatakayotupa dira nzuri ya kukuza na kuwaendeleza vijana na mchezo wenyewe wa soka.

Kikubwa ambacho nitahakikisha ntalisimia kidedea ni kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi, kuandaa makocha, waamuzi chipukizi na upatikanaji wa vifaa vya michezo ikiwemo kuhakikisha viwanja vya michezo havitumiki kwa matumizi mengine na hivi vilivyopo viweze kuboreshwa zaidi.

Lingine ni kuhakikisha mikoa yote nchini inapata haki sawa katika kugawiwa rasilimali zinazopatikana kutoka kwa wadhamini na Shirikisho la kandanda duniani (FIFA) na kuhakikisha mfumo wa kutumia tiketi za elektroniki unaanza kutumika mara moja.

Mfumo huo utasaidia kumaliza tuhuma za ubadhirifu wa mapato ya milangoni katika mechi mbalimbali zinazofanyika nchini katika viwanja mbalimbali.Zinapopatikana pesa kwa wingi ndio tutakapoweza kutumia fursa hiyo kufanya maendeleo ya mpira wa miguu.

Nafahamu majukumu mazito ambayo yanatakiwa kutekelezwa na kamati ya utendaji na nikiwa kama mjumbe nafahamu nchi yetu ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto mbalimbali katika uendelezaji wa michezo hasa mchezo wa soka.

Kwa miaka 13 iliyokaa Uingereza niliweza kupata nafasi ya kufanya kazi  (Part time) pale BBC Swahili kwa kweli niliweza kupata ufahamu  wa hali ya juu sana kuhusu mpira wa miguu na kufanya utafiti wa kina katika michezo ikiwa ni pamoja na wachezaji wake, viwanja, kanuni na mbinu mbalimbali.

Lakini mwaka 1999 niliweza kupata semina ya siku 45 nchini Brazili juu ya  uongozi wa mpira wa miguu (Football Administration), hatua ambayo ilinipata weledi mkubwa  sana katika uongozi wa mchezo wa mpira wa miguu.

Nina uhakika kwa hayo yote niliyoyapata kabla na baada ya kuondoka nchini, yameweza kunipa mwanga sahihi wapi tunapotakiwa kwenda, lakini pia kupata fursa ya kuweza kutumia uzoefu wangu na hiki nilichokipata kuweza kutumia ndani ya TFF.

Hivyo nimeamua kuingia TFF ili kutumia uzoefu wangu katika kuleta mabadiliko ya kweli, pamoja na kuwa mchezaji wa timu ya Pan African mwaka 1993, pia na mchezaji wa timu ya Taifa ya Vijana mwaka 1994.

Lakini kwa hivi sasa ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama Cha soka mkoa wa Pwani, Mjumbe wa kamati ya masoko ya TFF na Mwenyekiti wa Chaa Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA).

Read more
VITALI KLITSCHKO AMFUATA PACQUIAO, YEYE ATAKA URAIS

BINGWA wa uzito wa juu wa WBC raia wa Ukraine, Vitali Klitschko anataka kufuata nyayo za bondia mwenzake, Manny Pacquiao wa Ufilipino kwa kujiingiza kwenye siasa lakini yeye anautaka Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.

Manny Pacquiao pamoja na kuwa mbunge lakini pia anajishughulisha siasa na ni mbunge wa Bunge la Ufilipino, hali ambayo imemvutia Klitschko ambaye mwezi Agosti alisema lengo kubwa ni kuifanya Ukraine kuwa Ulaya, nchi ya kisasa yenye maisha ya kiulaya.


Anasema ataamua na watu wenye mtazamo mmoja, ndoto zinazofanana na kuingia kwenye siasa na kutokea ndani kufanya mabadiliko.
Read more
Alhamisi, 24 Oktoba 2013
PSG, BAYERN ZAUA UEFA, MAN UTD, MADRID ZASHINDA KWA MBINDE

LIGI ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi iliendelea tena jana katika viwanja nane tofauti kuwania nafasi ya kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Katika michezo hiyo timu za Bayern Munich na PSG walivuna ushindi wa mnene wa mabao 5-0 wakati Manchester United walishinda bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad huku Real Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Juventus.

Hapa chini ni matokeo ya michezo yote ya jana

Galatasaray                   3 - 1  FC Kbenhavn
Leverkusen                   4 - 0  Shakhtar Donetsk
Benfica                         1 - 1  Olympiakos
Bayern Mnchen           5 - 0  Viktoria Plzen
Manchester United      1 - 0  Real Sociedad
RSC Anderlecht           0 - 5  Paris Saint Germain
Real Madrid                 2 - 1  Juventus

CSKA Moscow            1 - 2  Manchester City

 Wachezaji wa Manchester City wakishangiliwa moja ya bao la Arguero
  Mshambuliaji wa Real Madrid akishangilia moja ya bao lake alilofungwa katika mchezo dhidi ya Juventus jana
 Mshambuliaji wa Galatasaray, Didier Drogba akishangilia bao lake alilofungwa katika mchezo wa jana
 Mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic akishangilia bao lake alilofungwa katika mchezo wa jana
 Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akimtoka kipa wa Juventus na kufunga bao la kwanza katika mchezo wa jana
 Wachezaji wa Manchester United wakishangilia bao la kujifunga la Real Sociedad katika mchezo wa jana

Read more
Jumatano, 23 Oktoba 2013
YANGA YAFANYA KWELI TAIFA, SIMBA YASHIKWA MKWAKWANI

KLABU ya Yanga jana iliwaliwaza mashabiki wake baada ya kuinyuka Rhino Rangers mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga ambao waliondoka na simanzi katika mchezo wa watani wa jadi Simba mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kukubali sare ya mabao 3-3, baada ya leo kurudisha mabao hayo matatu.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamis Kiiza dakika ya 12 baada yua kumalizia kazi nzuri ya Simon Msuva ambaye aliwatoka mabeki na kupiga krosi safi na kufanya timu hizo zinaenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa bao hilo moja.

Kazi nzuri ya Mrisho Ngassa ilizaa bao la pili baada ya pasi yake kumfikia Frank Domayo ambaye hakufanya ajizi na kukwamisha bao wavuni kwa shuti kali lilomshinda kipa wa Rhino, Mahamud Othman.

Pamoja na Kiiza kukosa mabao mengi lakini alijirekebisha na kukwamisha wavuni bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Ngassa ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 19 wakati watani wao Simba wamefikiwa pointi 20.

Simba ambao walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakikabiliana na Coastal Union walishindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa suluhu.

Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, David Luhende/Oscar Joshua, Kelivin Yondani, Mbuyu Twite, Rajab Zahir, Simon Msuva/ Nizar Khalfan, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza na Mrisho Ngassa.

Rhino Rangers: Mahamud Othman, Ali Mwanyiro, Hussein Abdallah, Julius Masonga, Ladslaus Mbogo, Stanslaus Mwakitos, Shija Mbogo, Oman Ndely/ Msafir Hamis, Victor Hangaya/Kamana Salum, Saad Kipanga na Nurdin Bakary.



Read more
YANGA NA RHINO TAIFA LEO, SIMBA KUONYESHANA KAZI NA COASTAL MKWAKWANI

YANGA na Simba kwa pamoja leo zinashuka katika viwanja viwili tofauti kupambana na Rhino Rangers na Coastal Union katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Bara.

Yanga ambayo ni mabingwa watetezi wenyewe watakuwa jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, kuvaana na Rhino ya Tabora inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JW).

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro amesema vijana wake wamefuta makosa na sasa wapo tayari kuikabiri Rhino Rangers leo.

“Kikosi kipo sawa kupambana na Rhino hapo kesho (leo), kama ni makosa tumeshayafanyia kazi na nadhani tutafanya vizuri zaidi katika mchezo huu na kilichobaki sasa ni muda kufika tuweze kuingia uwanjani,” anasema Minziro.

Yanga ilianza mazoezi juzi Jumatatu asubuhi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyora jijini Dar es Salaam baada ya Jumapili kutoka sare na Simba ya mabao 3-3 na Simba kwenye Uwanja wa Taifa.

Hadi sasa Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 katika michezo 9. Rhino yenyewe ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 7 katika michezo 9.

NAKO mjini Tanga, Simba inashuka dimbani leo mchana kupambana na Coastal Union ya mjini humo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekile Kamwaga ameuambia mtandao huu kwamba, kikosi cha Simba kiliwasili salama Jumatatu jijini Tanga tayari kwa mchezo huo wa leo na wachezaji Henry Joseph, Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud hawapo katika kikosi hicho.

“Timu imefika salama Tanga tangu Jumatatu mchana na hali ya kikosi kizima ni nzuri kinachosubiriwa sasa ni muda kufika ili tuweze kutazama pambano hili safi na la kuvutia kwetu sote, kwani Coastal ni timu nzuri ambayo ina wachezaji kadhaa ambao wamewahi kuwika na klabu mbalimbali za hapa nchini.

“Sisi kama Simba tunaamini tuna timu nzuri ambayo inaweza kupambana na timu yoyote na kutwaa ubingwa hivyo wakazi wa Tanga na miji ya jirani wajitokeze kwa wingi uwanjani kutazama pambano hili la kuvutia,” anasema Kamwaga.

Naye Mwenyekiti wa Coastal, Ahmed Aurora amesema kikosi cha timu yake kimejiandaa vya kutosha na hakuna tatizo lolote linaloikabiri timu yake kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba.

“Sisi tupo vizuri kabisa tunaisubiri Simba kwa hamu kubwa kuweza kupambana nao kwani tumejiandaa vizuri chini ya kocha wetu Joseph Lazaro ambaye amejiunga nasi hivi karibuni akichukua nafasi ya Ahmed Morocco.


“Tuna wachezaji wengi wazuri ambao wamewahi kutamba na timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, tunachohitaji sisi ni kufanya vizuri kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” anasema Aurora.
Read more
IJUE MICHEZO YA LEO YA UEFA


CSKA Moscow            v       Manchester City Arena Khimki     1:00 
Leverkusen                   v       Shakhtar Donetsk        BayArena  3:45 
Benfica                         v       Olympiakos        Estadio da Luz    3:45           
Manchester United      v       Real Sociedad     Old Trafford       3:45           
FC Bayern Mnchen     v       Viktoria Plzen    Allianz Arena     3:45           
RSC Anderlecht           v       PSG                    Vanden Stock     3:45           
Real Madrid                 v       Juventus        SantiagoBernabu     3:45           
Galatasaray                   v       FC Kbenhavn     Telekom Arena   3:45  
Read more