KLABU ya Yanga jana iliwaliwaza mashabiki wake baada
ya kuinyuka Rhino Rangers mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga ambao waliondoka na simanzi
katika mchezo wa watani wa jadi Simba mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya
kukubali sare ya mabao 3-3, baada ya leo kurudisha mabao hayo matatu.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamis Kiiza
dakika ya 12 baada yua kumalizia kazi nzuri ya Simon Msuva ambaye aliwatoka
mabeki na kupiga krosi safi na kufanya timu hizo zinaenda mapumziko Yanga
wakiwa mbele kwa bao hilo moja.
Kazi nzuri ya Mrisho Ngassa ilizaa bao la pili baada
ya pasi yake kumfikia Frank Domayo ambaye hakufanya ajizi na kukwamisha bao
wavuni kwa shuti kali lilomshinda kipa wa Rhino, Mahamud Othman.
Pamoja na Kiiza kukosa mabao mengi lakini
alijirekebisha na kukwamisha wavuni bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Ngassa
ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 19 wakati watani wao Simba wamefikiwa pointi 20.
Simba ambao walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa
Mkwakwani wakikabiliana na Coastal Union walishindwa kutamba ugenini baada ya
kulazimishwa suluhu.
Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, David
Luhende/Oscar Joshua, Kelivin Yondani, Mbuyu Twite, Rajab Zahir, Simon Msuva/
Nizar Khalfan, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza na Mrisho Ngassa.
Rhino Rangers: Mahamud Othman, Ali Mwanyiro, Hussein
Abdallah, Julius Masonga, Ladslaus Mbogo, Stanslaus Mwakitos, Shija Mbogo, Oman
Ndely/ Msafir Hamis, Victor Hangaya/Kamana Salum, Saad Kipanga na Nurdin
Bakary.
0 comments