KIKOSI cha Arsene Wenger kimeendelea kujichimbia
kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kushinda mchezo wake dhidi
ya Crystal Palace mabao 2-0 uliochezwa jana.
Kwa ushindi huo Arsenal wamefikiwa pointi 22
wakifuatiwa na Liverpool wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 20 nao
baada ya kushinda mchezo wao jana.
Mashabiki wa Arsenal walisubiri hadi kipindi cha
pili ndipo wainuke na kuanza kushangilia bao lao la kwanza kupitia kwa kiungo
mshambuliaji, Mikel Arteta kwa njia ya penalti kabla ya Olivier Geroud kufunga
kazi dakika chache kabla ya kipenga cha mwisho kulia.
Robin van Persie akiwa chini ya ulinzi wa wachezaji wa Stoke City
Katika mchezo mwingine Manchester United ilibuika na
ushindi kwa mbinde dhidi ya Stoke City wakiwa nyumbani na kufanikiwa kushinda
mchezo huo kwa mabao 3-2.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na ushindani
mkubwa, Stoke ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Peter Crouch
kabla ya Robin van Persie kusawazisha lakini mkwaju wa faulo wa Marko
Arnautovic uliomshinda kipa wa Manchester United, David da Gea na kujaa wavuni
na kuwafanya wenyeji waende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.
Mabao ya Wayne Rooney katika kipindi cha pili na
Chicharito ambayo yote yalifungwa kwa kichwa ndiyo yaliyopeleka shangwe Old Trafford
na kufanya Man Utd kuibuka na ushidni huo wa mabao 3-2.
Mshambuliaji wa Manchester United, Chicharito akifungao bao la tatu kwa kichwa
Nao Liverpool jana walifanya mauaji baada ya
kuikandamiza West Bromich mabao 4-1 huku Luis Suarez akionekana kurudi kwa kasi
na kufunga hart-trick wakati bao linguine lilifungwa na Daniel Sturridge na bao
la kufutia machozi la West Brom lilifungwa na James Morrison.
Matokeo mengine ya michezo iliyochezwa jana Everton
ikichezea ugenini imeifunga Aston Villa mabao 2-0. Norwich imetoka suluhu na
Cardiff City na Southampton ikaifunga Fulham mabao 2-0.
0 comments