Open top menu
Jumatano, 20 Novemba 2013
AFRIKA KUSINI WAWAFUNGWA MABINGWA WA DUNIA, ENGLAND YALALA TENA KWA UJERUMANI

TIMU ya Afrika Kusini imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa dunia, Hispania katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo usiku nchini Afrika Kusini.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Bernard Parker dakika ya 56 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo hayo na kuwaacha mabingwa hao ambao walikuwa wamekamilika uwanjani kutoambulia kitu.

Katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa uliozikutanisha timu za Ujerumani na England uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley ulimaliza kwa Three Lions kushindwa kulipa kisasi na kukubali kipigo cha bao 1-0.

England na Ujerumani walikutana kwa mara mwisho mwaka 2010 kwenye fainali za Kombe la Dunia na kukubali kipigo cha mabao 4-1 katika hatua ya robo fainali na kuyaaga mashindano hayo.


Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na beki wa Arsenal Per Martesacker katika ya 39 na kufanikiwa kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Read more
Jumanne, 19 Novemba 2013
ALGERIA WAARABU PEKEE KOMBE LA DUNIA BRAZIL KUTOKA AFRIKA

TIMU ya taifa ya Algeria leo usiku imekata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 na kuwa timu pekee ya kiarabu kutoka Afrika itakayoshiriki michuano hiyo mwakani.

Algeria wamefanikiwa kufuza kucheza fainali hizo baada leo usiku kuiondosha Burkina Faso katika mbio hizo baada ya kushinda mchezo kwao bao 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 3-3, hivyo wao kupenya na faida ya mabao ya ugenini. Mchezo wa awali Burkina Faso walishinda mabao 3-2.

Waarabu hao wametinga hatua hiyo na kuwaacha wenzao Misri iliyoondolewa na Ghana wakati Tunisia walitupwa na Nigeria katika hatua ya makundi.

Shujaa wa Algeria katika mchezo huo alikuwa Madjid Bougherra aliyeifungia timu yake bao pekee katika mchezo huo na kuikatia tiketi ya Brazil timu yake katika dakika ya 49.
Read more
GHANA YAFUZU SAFARI YA BRAZIL, YAPIGWA 2-1 NA MISRI

TIMU ya Taifa ya Ghana pamoja na kupoteza mchezo wake wa leo usiku dhidi ya Misri kwa mabao 2-1 lakini wamefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 za nchini Brazil, katika mchezo uliochezwa jijini Cairo, nchini Misri.

Ghana imefuzu hatua kwa jumla ya mabao 7-3 baada ya kushinda kwa ushindi mnono wa mchezo wa kwanza kwa mabao 6-1 mchezo uliochezwa jijini Kumasi.

Misri ambayo iliingia uwanjani ikiwa na nia ya kupata ushindi wa mabao 5-0 ili waweze kufuzu katika fainali hizo lakini walijikuta hadi wanaenda mapunziko wakiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Amr Zaki dakika ya 24.

Waarabu hao walikuwa na kasi katika kipindi cha pili wakisaka mabao manne lakini walilazimika kusubiri hadi dakika ya 84 ambapo Gedo aliongeza bao la pili kabla ya Kevin-Prince Boateng kuipatia Ghana bao la kufutia machoni katika mchezo huo dakika ya 89.


Ghana inaungana na Ivory Coast, Nigeria na Cameroon ambazo tayari zimeshafuzu hatua hiyo na wanaisubiri mshindi kati ya Burkina Faso na Algeria ambao unachezwa kwa sasa. Katika mchezo wa awali Burkina Faso walishinda mabao 3-2.
Read more
STARS FULL MZIKI WABANWA TAIFA, KIM HALI TETE

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu na Zimbabwe jioni hii katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Zimbabwe wangeondoka na sherehe Uwanja wa Taifa, kama si Refa Ronnie Kalema aliyesaidiwa na Samuel Kayondo na Lee Okelo wote kutoka Uganda kuwakatalia bao zuri lililofungwa na Sithole Simba dakika ya 90.

Kwa ujumla, Tanzania haikuwafurahisha mashabiki wake leo pamoja na kuwa na kikosi chake kamili, wakiwemo washambuliaji tegemeo Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wanaocheza TP Mazembe ya DRC, kiungo Mwinyi Kazimoto anayechezea Al Markhiya ya Qatar na beki Shomari Kapombe anayechezea AS Cannesd ya Ufaransa.
Stars iliuanza vyema mchezo huo, safu ya kiungo ikiundwa na chipukizi Hassan Dilunga aliyecheza pamoja na Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto.

Viungo hao waliweza kuwachezesha vizuri washambuliaji watatu wa Stars, Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, lakini wakashindwa kutumia nafasi hizo vizuri kipindi cha kwanza.
Zimbabwe walizinduka baada ya dakika 10 na kucheza vizuri, wakitengeneza nafasi pia ambazo walishindwa kuzitumia.

Safu ya kiungo ya Stars ilikufa ndani ya dakika 30 na Zimbabwe wakaanza kutawala mchezo. Kipindi cha pili, Kim alifanya mabadiliko ya viungo akiwaingiza Amri Kiemba na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuchukua nafasi za Kazimoto na Dilunga na kidogo Stars ilianza kutawala sehemu ya katikati ya Uwanja, lakini iliishia kukosa mabao ya wazi.

Nafasi ambayo Stars wataijutia zaidi ni ya dakika ya 75, kufuatia Kapombe kutia krosi nzuri baada tya kupokea pasi ya Sure Boy, lakini Ulimwengu akazidiwa na kipa Tapiwa Kapini aliyedaka mpira miguuni mwake.
Kipa Ivo Mapunda alifanya kazi nzuri kwa kuokoa michomo mitatu ya hatari hali ambayo ilifanya ashangiliwe baada ya mechi.
Mashabiki walimzomea kocha Mdenmark Kim Poulsen baada ya mechi wakimuambia timu imemshinda na kumtaka aondoke.


Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ivo Mapunda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/Himid Mao dk56, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Hassan Dilunga/Salum Abubakar dk51, Mwinyi Kazimoto/Amri Kiemba dk51, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk80.
Read more
KIBADENI, JULIO WATIMULIWA SIMBA, KOCHA WA GOR MAHIA, MATOLA WAKABIDHIWA TIMU

BAADA ya kumsimaisha mwenyekiti Ismail Aden Rage,kamati ya utendaji ya Simba imelivunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya kocha Abdallah king Kibaden na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio.

Kamati hiyo ya utendaji imefikia maamuzi hayo katika kikao cha jana ambacho pia kilikubaliana kumsimamisha mwenyekiti wao Rage mpaka mkutano mkuu wa wanachama utakapofanyika ambako anatakiwa kujieleza mbele ya wanachama.

Nafasi ya Kibaden na Julio sasa inachukuliwa na kocha wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya Zdravko Logaruzic raia wa Croatia ambaye atasaidiwa na Suleiman Matola aliyekuwa kocha wa Simba B.


Tokea mzunguko wa kwanza umemalizika mabosi wa Simba hawakuridhika na mwenendo wa timu yao na kikao cha jana kikafikia maamuzi hayo magumu.
Read more
YAMETIMIA, RAGE APIGWA STOP SIMBA

BAADA ya wanachama wa Simba kuhaha kutaka kumng’oa madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage sasa dua zao zimetimia baada ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kumsimamisha.

Kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kilifikia maamuzi hayo kutokana na madai ya kuwa kiongozi huyo wa juu wa Simba kukiuka miiko ya uongozi na kukiuka katiba ya klabu hiyo.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rage kuwasainisha mkataba wachezaji wawili kutoka Zanzibar Ally Badru na Awadh Juma aliyekuwa anacheza Mtibwa.

Mabosi wa Simba wamethibitisha kusimamishwa kwa Rage na muda huu wanazungumza na waandishi wa habari sababu za kuchukua maamuzi hayo magumu.

Taarifa ya awali inadai kuwa Rage amekuwa hajishughulishi kwa karibu na timu hiyo lakini pia amekuwa akikiiuka baadhi ya mambo ndani ya katiba na ndio maana kamati ya utendaji imepata nguvu ya kumsimamisha kwenye kikao hicho cha jana.


Baadaye tutakuletea taarifa za kina zaidi juu ya maamuzi hayo
Read more
HUKUMU YA MWISHO LEO, NI RONALDO AU ZLATAN KWENDA BRAZIL

MCHEZO wa leo kati ya Sweden na Ureno ndiyo utakaoamua ni staa gani kati ya Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic ataenda kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.

Mchezo huo wa marudio utachezwa kwenye Uwanja wa Solna jijini Solna nchini Sweden ambapo katika mchezo wa kwanza Sweden walikiubaki kichapo cha bao 1-0 liulilofungwa na Ronaldo katika mechi iliyochezwa jijini Instabul nchini Ureno.

Katika mchezo huo Sweden wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo na mshambuliaji na nahodha wake, Ibrahimovic atakapoa nafasi nya kushiriki fainali hizo.

Kocha wa Ureno, Paolo Bento ametamba kuibuka na ushidni katika mchezo huo na amewatahadharisha wapinzani wake kuwa kama watakuwa makini kumzuia Ronaldo basi wachezaji wengine watafunga tu na kuwapaleka Brazil.

Bento ambaye anauhakika na kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kushinda mechi ya kwanza na kuweza kumdhidhitibi nahodha wa Sweden, Ibrahimovici.

Michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali hizo itakayochezwa leo Ufaransa watakuwa na kibarua kigumu watakaporudiana na Ukraine mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Saint Denis.

Katika mchezo huo Ufaransa inahitaji ushindi ili waweze kufuzu kucheza fainali hizo za mwakani, timu hiyo ipo katika hali mbaya kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kipigo cha mabao 2-0.  


Mechi nyingine ni Romania watakuwa nyumbani kuwakaribisha Ugiriki kwenye Uwanja wa Bucharest, Croatia       watakuwa wenyeji wa Iceland kwenye dimba la Zagreb.
Read more
 MISRI ITAFANYA MIUJIZA LEO NA KWENDA BRAZIL? WANATAKIWA KUITUNGUA GHANA 5-0

NI muujiza pekee ndiyo utakaoupeleka timu ya taifa ya Misri katika fainali za Kombe la Dunia Brazil 2014, katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Ghana unaochezwa leo jijini Cairo.

Misri ili wafanikie kutinga katika fainali hizo na kuungana na Ivory Coast, Nigeria na Cameroon wanatakiwa kuifunga Ghana mabao 5-0 kutokana na kukubali kipigo cha mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Kumasi nchini Ghana.

Mshambuliaji wa Ghana, Asamoah Gyan amesema pamoja na kuibuka na ushindi mnono katika mchezo wa kwanza lakini lolote linaweza kutokea katika soka.

Mechi nyingine ambayo inatarajiwa kutoa timu ya tano ya Afrika itakayokwenda nchini Brazil katika fainali hizo, ni kati ya Burkina Faso ambao watakuwa ugenini kuvaana na Algeria.


Mchezo huo ambao unatarajia kuwa na ushindani mkubwa kutokana na mchezo wa kwanza kumalizika kwa Algeria kupoteza mchezo huo kwa kipigo cha mabao 3-2.
Read more
Jumatatu, 18 Novemba 2013