MCHEZO wa leo kati ya Sweden na Ureno ndiyo
utakaoamua ni staa gani kati ya Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic ataenda
kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.
Mchezo huo wa marudio utachezwa kwenye Uwanja wa Solna
jijini Solna nchini Sweden ambapo katika mchezo wa kwanza Sweden walikiubaki
kichapo cha bao 1-0 liulilofungwa na Ronaldo katika mechi iliyochezwa jijini
Instabul nchini Ureno.
Katika mchezo huo Sweden wanahitaji ushindi wa mabao
2-0 ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo na mshambuliaji na nahodha
wake, Ibrahimovic atakapoa nafasi nya kushiriki fainali hizo.
Kocha wa Ureno, Paolo Bento ametamba kuibuka na
ushidni katika mchezo huo na amewatahadharisha wapinzani wake kuwa kama
watakuwa makini kumzuia Ronaldo basi wachezaji wengine watafunga tu na
kuwapaleka Brazil.
Bento ambaye anauhakika na kuibuka na ushindi katika
mchezo huo baada ya kushinda mechi ya kwanza na kuweza kumdhidhitibi nahodha wa
Sweden, Ibrahimovici.
Michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali hizo
itakayochezwa leo Ufaransa watakuwa na kibarua kigumu watakaporudiana na Ukraine
mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Saint Denis.
Katika mchezo huo Ufaransa inahitaji ushindi ili
waweze kufuzu kucheza fainali hizo za mwakani, timu hiyo ipo katika hali mbaya
kutokana na kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kipigo cha mabao 2-0.
Mechi nyingine ni Romania watakuwa nyumbani kuwakaribisha Ugiriki kwenye Uwanja wa Bucharest,
Croatia watakuwa wenyeji wa Iceland
kwenye dimba la Zagreb.
0 comments