TIMU ya Taifa ya Ghana pamoja na kupoteza mchezo
wake wa leo usiku dhidi ya Misri kwa mabao 2-1 lakini wamefanikiwa kufuzu kucheza
fainali za Kombe la Dunia 2014 za nchini Brazil, katika mchezo uliochezwa
jijini Cairo, nchini Misri.
Ghana imefuzu hatua kwa jumla ya mabao 7-3 baada ya
kushinda kwa ushindi mnono wa mchezo wa kwanza kwa mabao 6-1 mchezo uliochezwa
jijini Kumasi.
Misri ambayo iliingia uwanjani ikiwa na nia ya kupata
ushindi wa mabao 5-0 ili waweze kufuzu katika fainali hizo lakini walijikuta
hadi wanaenda mapunziko wakiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Amr Zaki
dakika ya 24.
Waarabu hao walikuwa na kasi katika kipindi cha pili
wakisaka mabao manne lakini walilazimika kusubiri hadi dakika ya 84 ambapo Gedo
aliongeza bao la pili kabla ya Kevin-Prince Boateng kuipatia Ghana bao la
kufutia machoni katika mchezo huo dakika ya 89.
Ghana inaungana na Ivory Coast, Nigeria na Cameroon ambazo
tayari zimeshafuzu hatua hiyo na wanaisubiri mshindi kati ya Burkina Faso na
Algeria ambao unachezwa kwa sasa. Katika mchezo wa awali Burkina Faso
walishinda mabao 3-2.
0 comments