FIFA imethibitisha orodha ya majina ya wachezaji
watatu walioingia fainali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka
2013, Ballon d'Or ambao ni mtetezi Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck
Ribery.
Messi ameshinda mfululizo mara nne tuzo zilizopita,
lakini safari hii ni Ronaldo anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa mpira wa dhahabu.
Mshindi mtarajiwa, Messi anaweza kupokonywa tuzo
hiyo na Ronaldo kutokana na mchezaji huyo Real Madrid kuwa juu hivi sasa
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, amefunga mabao 32
tayari msimu huu kwa klabu na timu yake ya taifa, huku Messi kwa sasa yupo nje
ya kikosi cha Barcelona kutokana na maumivu ya nyama.
Mabao yake matatu aliyofunga peke yake, hat-trick
wakati Ureno inaifunga 3-2 Sweden katika mechi maalum ya kufuzu Kombe la Dunia,
yameongeza hamasa za watu kumpendekeza kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili katika
historia yake.
Ribery, aliyeiwezesha Bayern Munich kutwaa taji la
Ligi ya Mabingwa Ulaya, alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuishinda kabla ya
Ronaldo kufanya mambo makubwa dhidi ya Sweden na FIFA ikaongeza muda wa kupigia
kura washindani.
Mshindi atatangazwa katika usiku wa hafla maalum ya
Ballon d'Or mjini Zurich, Uswis Januari 13, mwakani.
Wakati huo huo, FIFA pia imethibitisha orodha ya
wachezaji wanaowania kuwamo katika kikosi cha wachezaji 11 bora wa dunia,
FIFPro World XI 2013.
Kuna wachezaji wanne wa England kwenye orodha hiyo
ambao ni Leighton Baines, Ashley Cole, Steven Gerrard na Wayne Rooney.
Wachezaji ambao wanatarajiwa kushindania kuingia
katika kikosi hicho ni:-
Makipa:
Gianluigi Buffon (Italy, Juventus); Iker Casillas
(Spain, Real Madrid CF); Petr Cech (Czech Republic, Chelsea FC); Manuel Neuer
(Germany, FC Bayern München), Víctor Valdes (Spain, FC Barcelona).
Mabeki:
David Alaba (Austria, FC Bayern München); Jordi Alba
(Spain, FC Barcelona); Dani Alves (Brazil, FC Barcelona); Leighton Baines (England,
Everton FC); Jérôme Boateng (Germany, FC Bayern München);Ashley Cole (England,
Chelsea FC); Dante (Brazil, FC Bayern München); Mats Hummels (Germany, Borussia
Dortmund); Branislav Ivanović (Serbia, Chelsea FC); Vincent Kompany (Belgium,
Manchester City FC); Philipp Lahm (Germany, FC Bayern München); David Luiz
(Brazil, Chelsea FC); Marcelo (Brazil, Real Madrid CF); Pepe (Portugal, Real
Madrid CF); Gerard Piqué (Spain, FC Barcelona); Sergio Ramos(Spain, Real Madrid
CF ); Thiago Silva (Brazil, Paris St-Germain FC); Raphaël Varane (France, Real
Madrid CF); Nemanja Vidić (Serbia, Manchester United FC); Pablo Zabaleta
(Argentina, Manchester City FC).
Viungo:
Xabi Alonso (Spain, Real Madrid CF); Gareth Bale
(Wales, Tottenham Hotspur FC/Real Madrid CF);Sergio Busquets (Spain, FC
Barcelona); Steven Gerrard (England, Liverpool FC); Andrés Iniesta (Spain, FC
Barcelona); Isco (Spain, Málaga CF/ Real Madrid CF); Mesut Özil (Germany, Real
Madrid CF/Arsenal FC); Andrea Pirlo (Italy, Juventus); Marco Reus (Germany,
Borussia Dortmund); Franck Ribéry (France, FC Bayern München), Arjen Robben
(Netherlands, FC Bayern München); Bastian Schweinsteiger(Germany, FC Bayern
München); Yaya Touré (Côte d’Ivoire, Manchester City FC); Arturo Vidal (Chile,
Juventus); Xavi (Spain; FC Barcelona).
Washambuliaji:
Sergio Agüero (Argentina, Manchester City FC); Mario
Balotelli (Italy, Manchester City FC/AC Milan); Edinson Cavani (Uruguay, SSC
Napoli/Paris Saint-Germain FC); Diego Costa (Spain, Club Atlético de Madrid);
Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid CF); Didier Drogba (Côte d’Ivoire,
Shanghai Shenhua FC/Galatasaray SK); Radamel Falcao (Colombia, Club Atlético de
Madrid/AS Monaco FC); Zlatan Ibrahimovi (Sweden, Paris Saint-Germain FC);
Robert Lewandowski (Poland, Borussia Dortmund); Mario Mandžukić (Croatia, FC
Bayern München); Lionel Messi (Argentina, FC Barcelona); Neymar (Brazil, Santos
FC/FC Barcelona); Wayne Rooney (England, Manchester United FC); Luis Suárez
(Uruguay, Liverpool FC); Robin van Persie (Netherlands, Manchester United FC).
0 comments