MSHIRIKI aitwaye Hope toka Burundi amejikuta
akianguka chini kwa mshituko wa furaha ulimkuta baada ya kuibuka kidedea kwa
kutangazwa mshindi wa Tusker Project Fame na kujinyakulia kitita cha Shilingi
5,000,000/= za Kenya.
Mashindano hayo yaliyomalizika hivi punde usiku huu
yamemwacha Hope katika taharuki huku akiwabwaga washiriki wenzake, Hisia
(Tanzania), Patrick (Rwanda), Wambura (Kenya), Daisy (Uganda), Amos & Josh
wa Kenya
Sauti ya pekee ya kijana huyo imeibua thamani yake
katika tasnia ya muziki, Hope hakuwahi kufanya video ya wimbo wowote zaidi ya
ule uliompatia ushindi wa Tusker.
.png)
By
13:08

0 comments