MECHI ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka
huu ya Kombe la Chalenji kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji
Kenya (Harambee Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos.
Kwa mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi
hiyo itachezwa Uwanja wa Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini
Nairobi. Mechi hiyo itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10
kamili jioni na itaoneshwa moja kwa moja
na kituo cha televisheni cha SuperSport kupitia chaneli ya SS9.
Kilimanjaro Stars imetinga hatua hiyo baada ya
kuivua ubingwa Uganda (The Cranes) kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya
robo fainali ya michuano hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji
la Mombasa.
Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo
zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho
Ngasa wakati katika mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba,
Athuman Idd na nahodha Kelvin Yondani.
0 comments