VUMBI LIGI KUU KUANZA KESHO, YANGA ‘WAZEE WA UTURUKI’ KUWAVAA ASHANTI TAIFA
MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi
nne zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti
United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo
Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa
Sugar kutoka Morogoro.
Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili
(Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa
shuhuda wa mechi kati ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande
wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es
Salaam.
Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga
vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani
vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh.
3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.