Open top menu
Jumatano, 1 Januari 2014

VINARA wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wamerudi katika nafasi yao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cardiff City uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.

Arsenal imeipiga kikumbo Manchester City ambao walikaa kileleni kwa saa moja baada ya kufikisha pointi 45 na kuwaacha City wakiwa na pointi 44.

Washika Bunduki hao wa London ilibidi wasubiri hadi dakika ya 88 baada ya mshambuliaji wake, Nicklas Bendtner kuwamisha mpira wavuni lakini dakika mbili baadaye Theo Walcott aliongeza bao la pili. 

Katika mchezo mwingine uliochezwa leo, Liverpool nao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City na kuwafanya kuchuka hadi nafasi ya nne kutoka nafasi ya tano, baada ya kufikisha pointi 39.

 Mabao ya Liverpool yamefungwa na Daniel Agger dakika ya 36 wakati bao la pili liliwekwa kimiani na Luis Suarez dakika ya 50 ya mchezo huo. 

Mabao ya Fernando Torres, Willian na Oscar yaliiwezesha timu ya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Southamptom katika mchezo uliochezwa mapema leo.


Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa mapema leo, Crystal Palace walitoshana nguvu na Norwich City baada ya kutoka sare ya mabao 1-1, Fulham leo imezinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United na Stoke City wamegawana pointi ya Everton kwa kutoka sare ya mabao 1-1, West Brom wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments