Open top menu
Alhamisi, 23 Januari 2014

MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' Amin na kundi la Sanaa la Makhirikhiri wa bongo ni miongoni mwa burudani zitakazosindikiza onyesho maalumu la 'Usiku wa Banza Stone’  la bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Wazee wa Kizigo.

Onyesho hilo maalum kwa ajili ya kumtambulisha mtunzi na mwimbaji wake Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anayerejea upya jukwanii Jumamosi hii ndani ya Meeda Club Sinza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na tayari Banza ameanza mazoezi makali ya kufua sauti yake tayari kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi waliokuwa wame-mis sauti na tungo zake. 

Kwa muda wa miezi mitatu Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishia kushindwa kupanda jukwaani kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  bendi hiyo lakini akalazimika kupewa mapumziko ili aweze kufanya mazoezi na kula kwa mpangilio ili aweze kuimarisha afya yake.

Alisema, Amin na Makhirikhiri wa Bongo ni sehemu  tu ya burudani zitakazopamba 'usiku wa Banza Stone' kwani kutakuwa na vikundi vingine vya sanaa vitakavyonogesha onyesho ambapo mara baada ya onyesho hilo wataendelea kumtambulisha Banza katika kumbi mbalimbali za burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya ziara nyingine katika baadhi ya Mikoa.


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments