Open top menu
Alhamisi, 9 Januari 2014

MTUNZI na mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo 'Next Level Wazee wa Kizigo' Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anatarajiwa kutambulishwa rasmi kurejea kwake upya jukwaan Januari 25 mwaka huu katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Meeda Club Cnza jijini Dar es Salaam.

Kwa muda wa miezi miwili Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya hivi karibuni kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na  Extra Bongo.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo Banza amepewa mapumziko maalumu ya wiki tatu kuimarisha afya yake na kufanya mazoezi tayari kujiandaa kurejea jukwaani kwa kishindo kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi waliokuwa waki -mis sauti na tungo zake.

“Tumeamua kumpa wiki tatu apumzike ambapo atazingatia kula vizuri, mazoezi binafsi sambamba na kupata muda wa kupumzika ili aweze kurudisha afya awe katika muonekano tofauti na sasa,” alisema.

Katika ziara ya Kanda ya Ziwa Banza alipata nafasi ya kuweza kuimba vipande vyake (mega mix) ingawa hakuweza kupewa nafasi ya kukaa muda mrefu stejini kutokana na afya kutoimarika vya kutosha.


Alisema, Extra Bongo kwa kutambua thamani ya afya ya mwanamuziki wake imeamua kumpumzisha Banza ili kujipanga kuwapa ujio wake mpya aliowaandalia wadau wa muziki wa dansi.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments