UFAMLE wa klabu ya Manchester United umezidi
kuporomoka baada ya kupokwa nafasi ya kwanza kuwa klabu tajiri duniani na
nafasi hiyo sasa inashikiriwa na Real Madrid ya Hispania.
Manchester United ambayo sasa ipo katika msimu mbaya
baada ya kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya England
lakini sasa imepoteza heshima ya nje ya uwanja.
Klabu hiyo ambayo ilikuwa nafasi ya kwanza mwaka
jana lakini sasa imetupwa mpaka nafasi ya nne, kwani nafasi tatu za juu
zimechukuliwa na Madrid, Barcelona ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani.
Madrid imeshika nafasi hiyo baada ya kuingia zaidi
ya euro 518 milioni katika msimu wa 2012/13, wakifuatiwa na Barcelona iliyoingia
euro 482 milioni wakati Bayern inashika nafasi ya tatu ikiingiza euro 431.
Nafasi ya nne ipo Manchester United iliyoingia euro
423 na Paris Saint-Germain ‘PSG’ ya Ufaransa imeshika nafasi ya tano kwa
kuingiza euro 398 milioni.
0 comments