SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF)
limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho
ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.
Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na
timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa
akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid
Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu
zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
0 comments