KIPUTE cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kinaanza leo
katika viwanja nane ambapo miamba 16 itavaana kuwania ushindi katika michezo hiyo
ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Katika michezo hiyo nane, macho ya mashabiki wa soka
duniani kote yatakuwa katika michezo kati ya Manchester United ya England na Bayer
Leverkusen ya Ujerumani mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Machezo mwingine ambao utavuta hisia za mashabiki wa
soka ni ule utakaozikutanisha timu za Galatasaray ya Uturuki ambayo itawakaribisha
Real Madrid kwenye Uwanja wa Turk Telekom
Arena.
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich watashuka uwanjani kuanza kutetea taji lao
dhidi ya CSKA Moscow mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Allianz Arena.
Olympiacos watawakaribisha Paris Saint German ‘PSG’ mchezo
utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karaiskakis wakati Benfica nao watakuwa nyumbani
kuwakabili Anderlecht kwenye
Uwanja wa Estadio da Luz.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Real Sociedad na Shakhtar Donetsk huu utapigwa kwenye Uwanja
wa Anoeta na FC Copenhagen watavaana na Juventus
kwenye Uwanja wa Parken.
Manchester City wao wataanza kampeni za Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Plzen mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Struncovy
Sady. Michezo yote itaanza saa 3: 45 Usiku.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo nane
ambapo ratiba yake itakuwa hivi
FK Austria Vienna v FC Porto
Franz
Horr
Atletico Madrid
v Zenit St Petersburg Vicente
Calderon
Barcelona
v Ajax Camp Nou
Marseille v Arsenal Stade Velodrome
AC Milan v Celtic
San Siro
Napoli v Borussia Dortmund San Paolo
Schalke 04
v Steaua Bucuresti Veltins
Arena
Chelsea v Basle Stamford Bridge
0 comments