Kiungo wa pembeni Gareth Bale akikabidhiwa jezi
namba 11 na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez
Klabu ya Real Madrid imevunja mzizi wa fitina baada
ya jana kumalizana na kiungo mshambuliaji, Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspur
kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya pauni 100 milioni.
Mchezaji huyo raia wa Wales amevunja rekodi ya
mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Cristiano
Ronaldo a mbaye alisajiliwa kwa ada ya uhamisho ya pauni 80 milioni mwaka 2009,
hivyo kufanya timu hiyo kuwa na wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa.
“Napenda kuwashukuru kila mtu katika klabu yangu,
Mwenyekiti, bodi, wafanyakazi wote,
kocha na wachezaji wenzangu na zaidi mashabiki ambao naamini watanielewa kwa
maamuzi ytangu ya ajabu ya kumaliza maisha yangu katika klabu yangu," alisema
Bale alipokuwa anazungumza na tovuti ya Tottenham.
“Nina uhakika kuwa huu ni wakati mzuri kuondoka
katika ambayo nilikaa vizuri na kucheza soka zuri katika siku zote zilizokuwa
pale. Najua wachezaji wengi wanapenda kujiunga na klabu bora yenye wachezaji
wenye vipaji, lakini ninachoweza kusema, ndoto yangu imetimia.
“Pamoja na kuondoka lakini Tottenham ipo moyoni
mwangu wakati wowote na nina uhakika msimu huu utakuwa wa mafanikio kwao. Sasa
naangalia mbele, kinachofuata katika maisha yangu ni kucheza soka katika klabu
ya Real Madrid.”
Wakati Madrid wakikamilisha kumnunua Bale
wamemruhusu kiungo wake, Kaka kutua katika klabu ya AC Milan ya Italia. Madrid
walikubaliana na Milan lakini walikuwa wakisubiri kukamilisha usajili wa Bale.
0 comments