NDOTO za mashabiki wa Manchester United za kumuona
mshambuliaji wao wa zamani, Crstiano Ronaldo akivaa tena jezi zao zimeyeyuka
leo asubuhi baada ya nyota huo kuongeza mkataba wa miaka mitano ya kuitumikia
klabu yake ya Real Madrid.
Ronaldo ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa ufikie
ukingoni mwaka 2015, mara kadhaa amekuwa akihusishwa na kurudi katika klabu
yake ya zamani ya Manchester United.
Nyota huyo wa Uren oleo asubuhi amesaini mkataba
mpya wenye thamani ya pauni 75 milioni (zaidi ya Sh 165 bilioni) lakini pia mtakaba
huo amekuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi nchini Hispania.
Tovuti ya klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu
imethibitisha kuingia mkataba na nyota huyo baada ya kukubaliana na mahitaji
yake ambayo sasa atakuwa analipwa zaidi kuliko wachezaji wote nchini humo.
Los Blancos hawajatoa wazi makubaliano yaliyomo
kwenye mkataba huo lakini wamethibitisha nyota huyo kuwa atalipwa zaidi kwani
katika miaka mitano ya mkataba wake atalipwa pauni 17 milioni (zaidi ya Sh 42.5
bilioni) kutokana na mshahara kamili atakaokuwa analipwa na klabu hiyo.
Kutokana na makubaliano hayo Ronaldo amewaacha mbali
wachezaji nyota kama Lionel Messi wa Barcelona na Gareth Bale aliyesajiliwa
hivi karibuni kwa usajili uliovunja rekodi ya dunia.
0 comments