MCHEZA tenisi namba moja kwa ubora duniani kwa
wanawake, Serena Williams jana alishinda taji lake la tano ya mashindano ya US
Open baada ya kumgalagalaza Victoria Azarenka katioka fainali ya mchjezo huo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Flushing Meadows.
Mwanadada huyo wa Kimarekani mwenye umri wa miaka 31,
alishinda mchezo huo kwa 7-5 6-7 (6-8) 6-1 ikiwa ni mara ya pili kukutana na
mchezaji huyo wa Belarusia.
Taji hilo ni la 17 kwa Serena ambaye sasa amefikia
rekodi ya Martina Navratilova na Chris Evert, hivyo kubakisha mataji saba
kumfikia anayeshikilia rekodi ya kuwa na mataji 24 iunayoshikiliwa na Margaret
Court's.
"Nilikutana na ushindani mkubwa sana, ni
mpiganaji mkubwa sana na hiyo ndiyo maana alistahili kushinda mataji makubwa
mawili," anasema Serema alipokuwa anamzungumzia Azarenka baada ya mchezo
kumalizika.
0 comments