WACHEZAJI wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi
katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam
FC ikiwa nyumbani.
Ahadi hiyo ilitolewa na wachezaji mbele ya viongozi
wao (Makocha Kaly Ongala na Ibrahim Shikanda, Mwenye kiti Said Muhammad, Katibu
Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele) kwenye kikao cha
pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini mwenendo wa timu hiyo baada ya
mechi nne za mwanzo za ligi kuu.
Wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na John Bocco,
Jabir Aziz na Salum Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika
mechi zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya
kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri nab ado ikashindwa
kupata matokeo. Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa kuanzia mechi ya leo ili
kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.
Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa
matokeo yaliyopita na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili
kurudisha makali yaliyoifanya Azam FC kuwa timu ya kuogopwa.
Azam FC itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC
ambapo katika mechi nne zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga.
Lakini timu zote mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na
idadi sawa ya pointi baada ya kucheza michezo minne kila moja, kusinda mmoja na
kutoka sare michezo mitatu hivyo kuwa na pointi sita.
Azam FC leo itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye
alipewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi
yake itajazwa na David Mwantika.
Kikosi kinachoanza leo ni
AISHI SALUM
ERASTO NYONI
WAZIRI SALUM
JOCKINS ATUDDO
DAVID MWANTIKA
HIMID MAO
KIPRE BOLOU
HUMPHREY MIENO
JOHN BOCCO
BRIAN UMONY
FARID MUSSA MALIK
0 comments