JANA klabu ya Manchester United ilianza vizuri
kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya
timu ya Bayer Leverkusen mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Mbali na ushindi huo lakini kupitia mchezo huo klabu
hiyo imeweka rekodi tatu muhimu kwa wachezaji wake pamoja na kocha wao ambazo
zimewafanya wahusika wake kulala usingizi mnono baada ya mchezo huo.
Rekodi ya kwanza iliyowekwa katika mchezo huo ni ya
mshambuliaji wa klabu hiyo, Wayne Rooney ambaye jana alifunga mabao mawili
katika ushindi huo na kumfanya aendelee kuwa mchezaji pekee wa England
aliyefunga mabao mengi katika michuano hiyo.
Rooney anashikilia rekodi hiyo baada ya jana
kutimiza mabao 29 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Paul Scholes aliyefunga
mabao 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Frank Lampard wa Chelsea
aliyefunga mabao 22 na Steven Gerrard yupo nafasi ya nne baada kufunga mabao
19, nafasi ya tano inashikiliwa na Andy Cole aliyefunga mabao 18.
Mchezaji mwingine ambaye jana ilikuwan siku yake
muhimu baada ya kumaliza mchezo huo ni kiungo mpya wa timu hiyo, Marouane
Fellaini ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa
na Manchester United
Fellaini hakuwahi kucheza mashindano hayo kwani
tangu alipotua Everton 2008 klabu hiyo haikuwahi kupata nafasi ya kushiriki
michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Mara baada ya mchezo huo Fellaini aliandika kwente ukurasa
wake wa Twitter: “Hii ni siku yangu muhimu sana. Nimetimiza ndoto yangu ya pili
katika maisha ya soka.” Ndoto ya kwanza kucheza katika klabu kubwa kama Manchester
United.
Pia kocha wa klabu hiyo, David Moyes ameweka rekodi
ya kurudi katika rekodi ya kukaa kwenye benchi wakati timu yake ikiwa
inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya miaka nane.
Mara ya mwisho alikaa kwenye benchi mwaka 2005 akiwa
na Everton baada ya kumaliza msimu wa 2004/05 ikiwa nafasi ya nne katika Ligi
Kuu ya England
0 comments