Hali ndani ya klabu ya Yanga ni tete, baada ya wazee
wa Yanga kutokubali maamuzi yaliyofanya na uongozi wa juu wa klabu hiyo chini
ya Mwenyekiti wake, Yussuf Manji.
Wazee hao
wakiongozwa na Mzee Ibrahim Ally Akilimali waliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani
kuwa hawakubaliani na kitendo cha uongozi wa Yanga kumuajiri Katibu Mkuu kutoka
Kenya pamoja na Mhasibu mwenye asili ya Kiasia.
Wazee hao walisema wamesikia kuwa Manji amemleta
katibu kutoka Kenya anaitwa Patrick Naggi anayechukua nafasi ya Lawrence
Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake na Mhasibu Mhindi, kitu ambacho
hawakubaliani nacho.
Wazee hao ambao ndiyo walioilaani klabu hiyo wakati
wa uongozi wa Lloyd Nchunga na kusababisha timu hiyo kuchapwa mabao 5-0 na
Simba katika mchezo wao wa mwisho katika misimu miwili iliyopita.
Kama mgogoro huo ukiendelea kuna uwezekano laana
hiyo ikarudi tena kwa klabu hiyo kwani wakati vuguvugu hilo likianza kufukuta
ni mwezi mmoja na siku kadhaa kabla ya kuchezwa mchezo wa watani wa jadi
uliopangwa kufanyika Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
0 comments