Naibu Waziri wa Utamaduni Vijana na Michezo, Amos
Makala (wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe Nahodha wa Topland ya Kinondoni, Dar
es Salaam, Omari Akida mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa
za mashindano ya Safari Pool 2013 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani
Morogoro
KLABU ya Top Land kutoka mkoa wa kimichezo wa
Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za
mashindano ya Safari Pool 2013, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani
Morogoro.
Top land walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga klabu ya
Mpo Afrika ya Temeke 13-10 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 5,000,000,
Kikombe na medali za dhahabu kwa kila
mchezaji.
Mshindi wa pili katika fainali hizo ni klabu ya Mpo Afrika ambayo ilizawadiwa Sh. 2,500,000
na medali za fedha kwa kila mchezaji wakati mshindi wa tatu ni klabu ya Supersport kutoka mkoa wa Manyala
ambao walizawadiwa Sh. 1,250,000 na medali za shaba na mshindi wa nne ni klabu
ya Mashujaa wa Ilala ambao walipata Sh. 1,000,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume (single),
mchezaji Festo Yohana kutoka klabu ya Mashujaa alitwaa ubingwa wa Taifa kwa
kumfunga Mussa Mkwega kutoka Morogoro 5-1 na kuzawadiwa Sh.700,000, kikombe na
medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alikuwa Mussa Mkwega aliyepata Sh. 350,000
na medali ya Fedha.
Mshindi wa tatu ni Mohamed Idd wa Atlantic ya Dodoma
ambaye alijizolea Sh 200,000 na medali ya shaba ambapo mshindi wa nne ni Ernest
John kutoka Tabora ambaye alizawadiwa Sh. 150,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake (Singles),
mchezaji Rose Deus kutoka Morogoro alitwaa ubingwa wa kitaifa kwa kumfunga
Cecilia Kileo kutoka Ilala 5-4 na hivyo Rose kuzawadiwa Sh 350,000 na kikombe
na medali ya Dhahabu ambapo Cecilia alikamata nafasi ya pili na kupata Sh 200,000
na medali ya Fedha.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji Merry Gumbu
kutoka Arusha ambaye alizawadiwa Sh 150,000 na medali ya shaba wakati Judith
Machafuko alishika nafasi ya nne na kuweka kibindoni Sh 100,000.
Hongera timu ya Top Land, najua mmewaonea ndugu zetu wa Mpo Africa, mwakani mjiandae kukutana na Kurasini City ya Temeke
JibuFuta