Klabu ya Simba ya Dar es Salaam leo imewapa burudani
mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Mafunzo ya
Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa
kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Septemba 14 mwaka
huu pamoja na kuwatambulisha wachezaji wake wapya, Amisi Tambwe, Henry Joseph na
Kaze Gilbert.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia wachezaji
wapya wa Simba waliwapa raha mashabiki wake kwa kuonyesha kiwango kizuri lakini
kiungo wake, Henry Joseph hakuonekana uwanjani kutokana kuwa katika kambi ya
Taifa Stars.
Mshambuliaji wake mpya, Tambwe alionyesha cheche
ikiwa ni sawa ni salamu kwa timu nyingine baada ya kuifungia timu yake mabao
mawili katika manne yaliyofungwa huku akitoa pasi ya bao linguine moja.
Mabao ya Simba yalifungwa na Tambwe mawili dakika ya
45 na 81, Sino Augustino dakika ya 47 na Said Nassor ‘Cholo’ dakika ya 83 wakati
mabao ya Mafunzo yalifungwa na Ally Juma dakika ya 32 na Jaku Juma dakika ya 52
na 72.
Simba SC; Anderw Ntalla/Abbel Dhaira, Nassor Masoud
‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Gilbert Kaze, Abdulhalim Humud
‘Gaucho’/William Lucian ‘Gallas’, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla, Amisi
Tambwe, Rashid Ismail/Sino Augustino na Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Zahor Pazi.
Mafunzo; Abdul Suleiman, Hamadi Hajji/Hajji Abdi,
Abdul Abdallah, Heri Salum, Said Mussa, Juma Othman/Haji Mwambe, Mohamed Abdul,
Masoud Hamad/Wahid Ibrahim, Juma Jaku, Ally Othman/Sadick Habib na Ally Juma.
0 comments