SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) wametoa ratiba
ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa timu za Afrika mwaka
ambapo raundi ya kwanza itachezwa Oktoba wakati mchezo wa marudiano itachezwa
mwezi Novemba mwaka huu.
Ratiba hiyo ambayo imejumuisha timu zilizofuzu hatua
ya makundi ambazo ni Ivory Coast, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Misri, Senegal,
Tunisia, Cameroon, Burkina Faso na Algeria.
Kwa mujibu wa hatua hiyo raundi ya kwanza itachezwa kati
ya Oktoba 11 na 13 wakati miamba hiyo itarudiana kati ya Novemba 15 na 19 mwaka
huu, michezo ambayo itakuwa imetoa wawakilishi wanne watakaoiwakilisha Afrika
katika fainali hizo zitakazofanyika nchini Brazil.
Ratiba hiyo iliyotolewa na Caf muda mchache uliopita
inaonyesha kuwa wawakilishi pekee wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,
Ethiopia watavaana na Nigeria, Misri watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Ghana.
Ivory Coast wamepangiwa na Senegal, Tunisia
watapepetana na Cameroon wakati Burkina Faso wanawania tiketi ya kucheza
fainali hizo dhidi ya Algeria.
0 comments