BONDIA Floyd Mayweather wa Marekani ameendeleza
rekodi yake ya kutoshindwa pambano lolote hadi sasa baada ya kumtwanga kwa
pointi poindia wa Mexico, Saul Alvarez katika mpambano uliofanyika Alfajiri ya
leo huko jijini Las Vegas, Marekani.
Bingwa huyo wa uzito wa light-middle mwenye umri wa
miaka 36, anashikilia mataji WBC na WBA, ameshacheza mapambano 45 na hajapoteza
hata moja hadi sasa.
Mayweather akimsukumia konde mpinzani wake katika mpambano huo
Katika mpambano huo wa raundi 12, Mayweather alipewa
ushindi ma majaji wawili na mmoja akimpa sare. Maamuzi hayo yalikuwa 114-114,
116-112, 117-111.
Ushindi huo wa Mayweather amevunja mwiko wa Alvarez
ambaye hakuwahi kupoteza mpambano wake katika mapambano 42 aliyopigana. Alvarez hili ni pambano
lake la kwanza kupoteza, hivyo kwa sasa ana rekodi ya kucheza mapambano 43 na
ameshinda 42 na kupoteza moja.
Alvarez akijibu mapigo ya Mayweather kwa kusukuma konde lililotua shavuni kwa bingwa huyo
0 comments