Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshare
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo
wake,Jack Wilshere atang'ara katika fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa
nchini Brazil, mwakani.
Kiungo huyo, 22 hakuonesha kiwango kizuri kwa taifa
lake wakati wa mechi yao dhidi ya Ukraine Jumanne iliyopita iliyomalizika kwa
kutoka suluhu.
Lakini Wenger alimtetea kiungo wake matokeo ya mechi
hiyo na kwamba ana uwezo na tabia zinazofanana na kiungo wa Ufaransa, Zinedine
Zidane kuwa kiungo tegemezi kwa taifa hilo.
"Kama Jack Wilshere atacheza kama anavyocheza
akiwa Arsenal tunaweza kusema poa, leo hakuwa katika kiwango chake, lakini
anavyocheza hivyo katika timu ya taifa kila mmoja ana hoji uwezo wake,"
alisema Wenger.
"Timu ya taifa siku zote huhitaji watu ambao wanaweza
kuhimili presha hizo, sisi (Wafaransa) tulikuwa naye Zidane ambapo Ufaransa
ikicheza vizuri ujue ni Zidane huyo
lakini wengine wanaweza lakini si kama Zidane.Tunahitaji vizazi vipya lakini
pia kuwa na aina ya kipekee ya mchezaji."
"Tuwe wakweli.Jack anaweza kufanya hiyo kazi.Ni
kijana,22, ana uwezo wa kufanya hivyo lakini anahitaji kucheza miezi sita bila
ya kuwa na majeruhi au tatizo lolote."
"Jack ana kila sababu ya kuwa juu, mchezaji wa
juu.Amepitia mazingira
magumu," kocha huyo aliongeza.
0 comments