KIUNGO wa Chelsea, Juan Mata amesisitiza kwamba hana
wasiwasi kugombania namba katika kikosi hicho na kwamba ataendelea kuitumikia
timu hiyo.
Willian amekuwa kiungo mpya mshambuliaji katika
kikosi cha kocha Jose Mourinho baada ya kusajiliwa kwa Andre Schurrle na kurudi
kwa Kevin de Bruyne aliyekuwa kwa mkopo Werder Bremen.
Victor Moses amejiunga kwa mkopo wa muda mrefu
Liverpool lakini Oscar naEden Hazard wameendelea kuwa wachezaji muhimu katika
kikosi hicho cha Stamford Bridge, na Mata amekuwa si mchezaji wa kikosi cha
kwanza tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini yupo
vizuri na anafanya mazoezi lakini amekumbana na wimbi la wachezaji wengi vijana
wenye vipaji kitu kinachofanya apate ushindani kutokana na wachezaji hao.
"Nia yangu haijabadilika.Nitakuwa mzuri kama
nilivyokuwa katika misimu mwili iliyopita na ikiwezekana nizidi zaidi kuwa
mchezaji bora."
Kiungo wa Hispania aliiambia Sky Sports kwamba:
"Ninafikiri ni vizuri kwa klabu, kwa kikosi na kwa meneja.
"Ninafikiri ni wazuri - De Bruyne, Schurrle,
Willian, ni wachezaji wadogo na ni bora.Kila mmoja ana nafasi yake, ana ufundi
wake na ninachoamini wote hao watatupa makubwa na ni vizuri tukawa na kikosi
cha ushindani.
"Ningetarajia tungecheza wote sita lakini
haiwezekani.Lakini ni vizuri kwa klabu katika mashindano yote tutakayoshiriki
msimu huu."
Aliulizwa kwamba anaweza kucheza kama ilivyokuwa
awali mara kwa mara, Mata alijibu: "Nina uhakika kwa hilo.Niwe muwazi
imekuwa ngumu tangu niwe majeruhi, hivyo ninafanya mazoezi kidogo na wenzangu
lakini sasa ninajisikia vizuri na ninaangalia mbele zaidi kucheza.
"Nitafanya kila niwezalo niwe kama misimu
miwili iliyopita na nitajaribu kufunga, kutengeneza na timu ishinde."
Alipoulizwa kwamba Mourinho atarajie nini kutoka
kwake,Mata alisema: "Tulizungumza kuhusu hilo na akasema nina umuhimu
kwake na katika kikosi, kwahiyo nia yangu ipo pale pale.Ninatakiwa kuwa mzuri
kama nilivyokuwa."
Mata alihusishwa kuondoka timu hiyo wakati wa
kipindi cha usajili kilichopita lakini alisema hakutilia maanani hizo tetesi na
hakufikiria kuondoka.
0 comments