Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha
mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu
jijini Banjul.
Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo
iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini
ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka
huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba
3 mwaka huu) itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa
Kumbukumbu ya Karume.
0 comments