BINGWA ya dunia wa mita 200, Mjamaica Usain Bolt amesisitiza
kuwa anatendelea kukimbia mbio za umbali huo katika michuano ya Jumuiya ya
Madola mwakani.
Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa Olimpiki anatarajia
kushiriki michuano hiyo itakayofanyika mwakani katika mji wa Glasgow, lakini
ataatoa uamuzi baada ya kujadiliana na Kocha wake, Glen Mills.
"Mbio hizo zipo katika mipango yangu," alisema
Bolt, 27. "Natamani sana kushiriki lakini siwezi kwenda kinyume na kocha."
Mjamaica huyo alisema pamoja na kuzimudu mbio za
mita 100 na 200 aliongeza: "Najisikia vizuri kukimbia mita 200, kama
nikienda nitafanya hivyo kwa kuwa hizo ndiyo chaguo langu."
Bolt hajawahi kutwaa medali ya dhahabu ya michuano
ya Jumuiya za Madola lakini alisema: "Tunaenda kujadiliana na kocha wangu,
hatuna uhakika zaidi kama tutaenda kujadili na kuona kama kuna umuhimu wa
kushiriki."
0 comments