MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Mganda Hamis Kiiza
amerejea kundini juzi usiku na leo amejiunga na mazoezini na uwezekano akaanza
kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Azam Jumapili.
Kiiza ambaye hajaitumikia klabu hiyo tangu kuanza
kwa msimu huu baada ya kuwa nchini Lebanon kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili
lakini nyota huyo aliporudi aliunganisha kwao Uganda na huko alijiunga na timu
yao ya Taifa.
Mshambuliaji huyo amejiunga na wachezaji wenzake
katika mazoezi ya leo asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari
ya Loyola na anaweza kutumiwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi
ya Azam Jumapili.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ameiambia
Nyumba
ya Michezo na Burudani, alisema atamuangalia nyota huyo katika mazoezi
ya kesho asubuhi kabla ya kuamua kumtumia katika mchezo wa Jumapili dhidi ya
Azam.
Brandts alisema mazoezi ya kesho ndiyo yatatoa
kikosi cha Jumapili na siyo kwa kumuangalia Kiiza peke yake. Akiona kama
mshambuliaji huyo yupo fiti kwa mchezo huo atamtumia lakini aliporidhishwa naye
ataanzia benchi.
0 comments