Bondia wa Tanzania, Francis Cheka ambaye
alikuwa bingwa wa IBF katika bara la
Afrika uzito wa kati (Super Middleweight) ameingia kwenye orodha ya mabingwa wa
dunia iliyotolewa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika IBF.
Cheka ameingia katika rekodi hiyo baada ya kumtwanga
bondia kutoka Marekani, Phil William na kutawazwa kuwa bingwa wa dunia
anayetambuliwa na Shirikisho la Ngumi la Dunia (WBF).
Ushindi wa Cheka sio tu kwa Tanzania bali na kwa
bara la Afrika na dunia yote kwa ujumla. Cheka ameungana na mabingwa wengine wa
dunia wa uziro wa kati (Super Middleweight) wanaotambuliwa na vyama na mashirikisho
kadhaa.
Orodha hiyo ya mabingwa na mataji yao kwenye mabano
ni Carl Froch wa Uingereza (IBF), Andre Ward wa Marekani (WBC), Andre Ward wa Marekani
(WBA), Robert Stieglitz wa Ujerumani (WBO) na Thomas Oosthuizen wa Afrika ya Kusini (IBO).
Ushindi wa Cheka umeifanya Afrika kuwa na mabondia
wawiliu waliongia kwenye orodha hiyo kwani awali alikuwa Thomas Oosthuizen
kutoka Afrika ya Kusini.
0 comments