Wakati pazia la usajili barani Ulaya limefungwa jana
saa saba usiku kila timu ilikuwa ikihaha kuwania saini za wachezaji wanaowataka
katika msimu huu.
Katika mbio hizo timu ya Manchester United ambayo
imekuwa ikihaha kuimarisha katika nafasi yake ya kiungo, imefanikiwa kumnasa kiungo
wa Everton, Marouane Fellaini dakika za mwisho kabla ya usajili huo kufungwa.
Manchester United imefanikiwa kumnasa Mbelgiji huyo
kwa ada ya uhamisho wa pauni 27.5 milioni (zaidi ya Sh 60 bilioni) na kmuungana
na meneja wake wa zamani David Moyes.
Manchester United pia wamewakosa wachezaji Ander
Herrera wa Athletic Bilbao, Sami Khedira na Fabio Coentrao wote wa Real Madrid.
Moyes alisema: "Nimefanya kazi ya Marouane kwa miaka
mitano na nimefurahi kwa uamuzi wake aliochukua wa kujiunga na Manchester
United. Kiungo huyu huwa anacheza kwa uwezo mkubwa na natumaini ataleta
mabadiliko katika kikosi changu."
Pia Arsenal wamefanikiwa kumnasa kiungo mshambuliaji
wa Real Madrid, Mezus Ozil kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa klabu hiyo
wa pauni 42.5 milioni (zaidi Sh 103 bilioni).
Muda mchache kabla ya usajili kufungwa klabu ya
Everton waliwasaini wachezaji Romelu Lukaku akitokea Chelsea, James McCarthy wa
Wigan na kiungo wa Manchester City, Gareth Barry.
West Brom nao wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji
Stephane Sessegnon na Victor Anichebe wakitokea katika klabu ya Sunderland,
Wakati Cardiff City wamemsajili Peter Odemwingie na Fabio Borini wa Liverpool na
Andrea Dossena wamejiunga Sunderland kwa mkopo.
0 comments